Uchaguzi 2020 Kasulu: Dkt. Magufuli aahidi Kigoma kuwa kama Ulaya

Uchaguzi 2020 Kasulu: Dkt. Magufuli aahidi Kigoma kuwa kama Ulaya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli amesema maendeleo hayana chama lakini unachagua chama na kiongozi atakayekuletea maendeleo ya kweli

916C7DB9-148E-4951-8DFA-13B9A98C4854.jpeg

Ameyasema hayo alipokuwa Kasulu, katika harakati zake za kuomba kura kwa wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020. Amesema atawejengea lami itakayotoka Kigoma mpaka Nyakanazi, kwa kile alichosema wapinzani ‘waisome namba’

8DEC7E86-A278-4B96-9D45-5BB6A1971066.jpeg

Amesema lazima Kigoma ibadilike iwe kama Ulaya katika mipango wameweka Tsh bilioni 402 ili kuiendeleza Kigoma ili wageni kutoka nchi mbalimbali wapite Kasulu kisha wawe na uamuzi wa kutumia njia hizo

952D7D0A-5969-4381-BFFD-CA39812A2FF8.jpeg

Amesema hiyo itafanya biashara kukua kiasi cha wanawake kuweza kupata wanaume hata wa Afrika Kusini ambao watawagea dola. Na wanaume watapata wachumba wazungu




Rejea: By 2015 Kigoma kuwa kama Dubai, Mwanza kuwa kama California
 
CCM na TANU Baba yake wapo madarakani kwa miaka mingapi sasa? Kigoma haikuwepo? Ilikuwa imezama Ziwa Tanganyika! Bwana huyo asifie wanawake wa Kigoma aende zake. Hana jipya Ila wananchi tuna JAMBO LETU tarehe 28/10/2020.
 
Daaah, kweli amechanganyikiwa miaka mitano ameitelekeza Kigoma Leo ndio ataweza?
 
Back
Top Bottom