Uchaguzi 2020 Kasulu: Dkt. Magufuli aahidi Kigoma kuwa kama Ulaya

Uchaguzi 2020 Kasulu: Dkt. Magufuli aahidi Kigoma kuwa kama Ulaya

Rais wa nchi hii ajae lazima kuhakisha mikoa yote iliyo karibu na nchi jirani inakua na uchumi wa kutosha kulisha nchi jirani, tz ni tajiri but hatuna mikakati ya kiuchumi ,kwa Nini tushindwe kuweka bandari kavu n.k

Katika mikoa husika ,kwamba sio lazima magari au mizigo kwenda nchi jirani ichukuliwe dar yatubidi kujipanga , so rais ajae ambae mungu ameisha mchachagua na anamjua kuliko binadam yoyote itakubidi zingatia haya
 
Mkoa umesahaulika

Barabara zote, zipo hovyo kuna vumbi jekundu halifai

Kila mwaka anakuja anahidi, utekelezaji ni zero

Barabara ya nyakanazi hadi kibondo ni vumbi tupu, Ndio maana funza zimezagaa ccm ipo tu inaahidi kila awamu

Barabara kibondo hadi kasulu ni shida tu, haifai, ahadi hewa kila awamu

Yupo busy na chato,dsm na huko kwingine

Kgoma mkimpa kura JPM, nadhani mtakuwa mnadhidi kujiionesha namna gani mlivyo wa hovyo.

Ni Rais wa Barabara na madaraja lakni, Kigoma miundombinu ni zero,

Uzi tayar
 
Naona askari jela wa The Hague wanamtamani mfungwa mpya
 
Naona kama Lissu karahisishiwa hapa. Maana ni kiasi cha kuwakumbusha ahadi ya Dubai tu ya 2015 kama imeyeyukia wapi hata leo itolewe ahadi ya Ulaya. Yaani wanakigoma mmekuwa cheap kiasi hicho??
 
Amesema hiyo itafanya biashara kukua kiasi cha wanawake kuweza kupata wanaume hata wa Afrika Kusini ambao watawagea dola. Na wanaume watapata wachumba wazungu




Ikiwa kama kweli Rais wa nchi amesema haya basi hii ni dhihaka ya juu kweli. Kwanza kabisa tujiulize ni kwa nini haya anayoahidi sasa kwa nini hakuyafanya katika miaka mitano alokuwepo madarakani? Na kwa nini sio tu kutofanya bali kwa nini alishindwa hata kujaribu kuyafanya katika miaka mitano iliyopita.

Hii ni dhihaka na dharau kwa wananchi pale Rais anapoamini maendeleo na furaha ya wananchi wake ni kupata waume wa afrika kusini, kugawiwa dola na kupata wachumba wa kizungu! Hii ni aibu na inaonyesha dhahiri ni namna gani Rais hajui yanawakera wananchi wake na nini wanachokihitaji katika maisha yao ya kila siku.

Watanzania tunakwenda wapi jamani!!!!!!
 
Bora angesema taifanya iwe Kama dar, ahadi za wanasiasa Ni sawa na zile za kumtongoza demu ili utimize haja
 
Aisee hii itakua vzr sana,machalii wa kigoma wamechoka kutoa funza miguuni aiseee.
 
..jana kuna mchangiaji hapa JF nilimwambia Magu hawezi kufanya mikutano miwili bila kuwazungumzia vibaya na kuwadhalilisha wanawake.
Hilo neno "kudhalilisha" unalitumia vibaya

Kajaribu kuangalia maanake na mahali linapotumika
 
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli amesema maendeleo hayana chama lakini unachagua chama na kiongozi atakayekuletea maendeleo ya kweli


Ameyasema hayo alipokuwa Kasulu, katika harakati zake za kuomba kura kwa wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020. Amesema atawejengea lami itakayotoka Kigoma mpaka Nyakanazi, kwa kile alichosema wapinzani ‘waisome namba’


Amesema lazima Kigoma ibadilike iwe kama Ulaya katika mipango wameweka Tsh bilioni 402 ili kuiendeleza Kigoma ili wageni kutoka nchi mbalimbali wapite Kasulu kisha wawe na uamuzi wa kutumia njia hizo


Amesema hiyo itafanya biashara kukua kiasi cha wanawake kuweza kupata wanaume hata wa Afrika Kusini ambao watawagea dola. Na wanaume watapata wachumba wazungu




Rejea: By 2015 Kigoma kuwa kama Dubai, Mwanza kuwa kama California

Hivi ile bandari ya kibirizi ilishakuwa kama Dubai toka enzi wameahidi hivyo? Daaah maccm wasahaulifu aisee!!!
 
Back
Top Bottom