Kasumba kikwazo katika maendeleo ya Kijana

Kasumba kikwazo katika maendeleo ya Kijana

Thinkerboytz

New Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Na Betuel John

Katika ulimwengu wa sasa mafanikio ya watu wengi maarufu na mashuhuri yamekuwa yakiwavutia sana watu wengi hasa vijana ambao kwa kiasi kikubwa ndio wanaohangaikia ndoto zao za kuwa na maisha mazuri na mafanikio.

Katika kuhangaikia ndoto hii vijana wengi wamejikuta wakisahau malengo na ndoto zao na kukimbilia ndoto za watu wengine ikiwemo kuiga mitindo mbalimbali ya maisha ya watu wengine wakiamini kuwa kufanya hivyo kutawafanya wawe na maisha mazuri kama hao jambo ambalo sio kweli.

Kasumba inatesa vijana, ni rahisi kijana leo hii kujiingiza katika michezo ya kubeti kwa lengo la kupata utajiri wa haraka kuliko kujiingiza katika masuala ya kilimo na ufugaji kwa kuamini kuwa shughuli hizi ni za wazee na watu wa ngazi ya chini,na ndiyo maana idadi ya vijana imekua kubwa katika betting, online marketing kuliko kwenye kilimo na ufugaji au pengine hata biashara ndogondogo.

Mawazo kama “nikifanya hivi nitaonekaje?”, “mbona flani kafanikiwa bila kufanya hivi" hizi ni kauli za kujipa moyo lakini zenye kurudisha nyuma ari ya kupambana kufikia malengo. Katika kufanikiwa tusiweke “ubrazameni" na “usistaduu" kwa maana kuwa tusichague kazi za kufanya kwa kuangalia watu wengine watakuonaje

Kasumba ni hatari, kijana mwenzangu jifunze kupitia wengine lakini katu usiruhusu mitindo yao ya maisha kubadili mtizamo wako katika kutafuta mafanikio. EPUKA KASUMBA, Amini katika mawazo na ndoto zako bila kuchagua kazi.
 
Kuliko kuiga kilimo na shughuli zingine ambazo wazee wamezifanya tangu na tangu bila mafanikio, ni kheri vijana kujaribu mbinu mpya.
 
Back
Top Bottom