Mwaka 2006 kuna mwanangu alipata Syphilis ikapelekea hadi kupata vipele fulani vyenye usaha kichwani. Kuna rafiki yetu ni daktari alikuwa anaenda kumchoma sindano home kwake, jamaa alikuwa analia kama mtoto na kugalagala chini akisema zinauma sana. Bahati mbaya sasa, binti aliyempa ule ugonjwa alikuwa anatokea ushuani yani, pisi kali kwelikweli.
Kuna mwanangu mwingine alipata gono, bahati mbaya sana mke wake akafahamu akaja kulalamika kwetu akitishia talaka. Jamaa anaumwa, mke kakazana amtaje huyo mwanamke aliyelala naye. Akatishia kuyapeleka kwa wazazi. Binti aliyempa ule ugonjwa ni mzuri na huwezi hata kumdhania aisee. Ilikuwa ni balaa juu ya balaa...
Baada ya haya matukio kutokea, niliamini kwamba Looks can be deceptive....
Ukihangaika sana na hawa mabinti unaweza hata ukapata matatizo na mikosi tu....