A
Anonymous
Guest
Mimi ni mmoja wa wamiliki wa maeneo ya viwanja na nyumba yaliyopo Kata ya Mbezi, Kijiji cha Msufini Kidete, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani.
Maeneo yetu yamekuwa yakihitajika na wawekezaji kutoka China wanaopanga kujenga kiwanda cha kutengeneza nondo. Hata hivyo, kinachotutia wasiwasi ni bei iliyowekwa na Serikali kwa kushirikiana na wawekezaji hao kwa ajili ya ununuzi wa maeneo yetu.
Tunaelezwa kuwa bei iliyowekwa ni Shilingi 9,500 kwa mita moja ya mraba, huku baadhi ya viongozi wakitutaka tukubali bei hiyo kwa hoja kwamba wengine tayari wamekubali na kwamba kiwanda kitajengwa hata kama baadhi yetu hatutauza.
Kwa kuzingatia thamani ya ardhi kwa sasa na maendeleo yanayotarajiwa katika eneo hilo, tunaona bei hiyo kuwa ndogo na isiyoendana na thamani halisi ya maeneo yetu.
Tunaomba mamlaka husika zitoe ufafanuzi kuhusu utaratibu uliotumika kufikia bei hiyo, pamoja na kuhakikisha wamiliki wa ardhi wanapata thamani stahiki ya maeneo yao kabla ya ardhi kuchukuliwa kwa ajili ya uwekezaji.