Kataa ndoa tunakemea ufungaji wa ndoa, kipindi hiki kikali cha talaka na mgawanyo wa mali

Kataa ndoa tunakemea ufungaji wa ndoa, kipindi hiki kikali cha talaka na mgawanyo wa mali

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
46,398
Reaction score
102,530
Salaam wakuu, kwanza naomba ifahamike kataa ndoa ni chama chenye kulinda haki na maslahi ya jinsia zote zinazo tambulika kisheria.
(me na ke).

Chama hiki kilianzishwa baada ya kushamiri kwa upigaji, ukandamizaji wa haki na ufekiji wa hisia ili kujitengenezea mazingira ya kumdhurumu au kumdhuru mwingine katika taasisi ya ndoa.

Mimi kama katibu mwenezi wa kataa ndoa, naendelea kuwakumbusha kuendelea kuwa macho dhidi ya hisia feki, mahusiano feki na mitego yote itakayo tumika kukuingiza kichwa kichwa katika ndoa.

Maana kipindi hiki talaka ni nyingi mno, kugawana mali ambazo ni jasho la mtu mmoja lime shamiri sana kudadadeki.

Watu wanalia na kusaga meno huko kwenye ndoa, ni vile wana roho za paka wanaona wafe na tai shingoni.

Kataa ndoa linda maisha yako,
Kataa ndoa linda uhuru wako,
Kataa ndoa linda mali zako.

Soma pia :
Mjadala kwa wanaokubali kuoa (Ndoa)

Screenshot_20250925-021750_1.jpg
​
 
Nahimiza wale wanaofunga ndoa wafunge wakiwa tayari kufunga ndoa.

Na wale wanaofunga ili waonekane wameoa na kuolewa, na wale wanaofunga huku wakipiga hesabu za zawadi na pesa wenyewe waendelee kulia wapigane matukio wapeane talaka watakuwa wenyewe.
 
Naam ndoa ni kwatu sahihi, na ndoa zenye maana zilikuwa zile za watu wa 1940- 1980.

Huku kwingine ni kujaribu kuikausha bahari, kwa tisheti ya ccm.
 
Ndoa ni makubaliano ya Mwanamke na Mwanaume kuishi pamoja au kua na mapenzi ya pamoja,mapenzi ambayo yanatambuliwa na Polisi na Mahakama,

Watu hao hukubaliana kuishi pamoja na kutatua matatizo yatakayo tokea kwenye maisha yao ya ndoa,matatizo ambayo yasingetokea kama wasingeoana.
 
"matatizo ambayo yasingetokea kama wasingeoana.":😅😅😅
 
Back
Top Bottom