The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Nimekuwa nikisoma kampeni chafu na uchwara za kataa ndoa zinazosambazwa na kutangazwa humu. Sifichi msimo wangu.
Nachukia wale wote wanaokataa ndoa na kutaka kulazimisha wengine. Kama wanazikataa tokana na matatizo yao fichi, ni haki yao.
Lakini wasilazimishe wengine. Nami hapa silazimishi zaidi ya kutoa fursa na uwanja kwa wapenzi wa ndoa kujitetea na kujitangaza kujibu huu utumbo, ulimbukeni, na uzwazwa wa kataa ndoa.
Kama wewe ni rijali kweli, unawezaje kukataa ndoa? Ili iweje na ufanye au kufanywa nini jamanini wanangu?