Nahisi kuna watoto wameachiwa swichi hapo tanesco maana siku za mechi lazima umeme utakatika tu haswa timu ya Bongo ikiwa inafanya vizuri hizi za watani, hua najiuliza profesionalizm iko wapi.. Nchi zingine umeme ukikatika watu wanaandika ripoti za maana na ikionekana kuna uzembe, wanawajibishwa ila huku kwetu ukisikia kuna Mechi ya Watani basi hakikisha simu yako imejaa chaji maana siku iyo lazima umeme ukatike, Siku nikipewa cheo hata cha Unaibu waziri kumaanisha! Kuna watu wataonja joto ya jiwe.. upumbavu kama huu siwezi kuuvumilia