Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katika uzinduzi wa kampeni za udiwani Kata ya Nyakaliro, Jimbo la Buchosa mkoani Mwanza, Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Sengerema na mmoja wa wasimamizi wa kampeni Jimbo la Buchosa, Comrade Boniphace Katalyeba, amewasihi wananchi wa Buchosa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo, Eric James Shigongo, kutokana na maendeleo makubwa yanayoendelea kuletwa katika eneo hilo.
Katalyeba amewataka wananchi kuachana na sera za upinzani zisizo na tija, akizitaja kama “sera za ubwabwa” za mgombea ubunge kupitia Chama cha CHAUMMA, akisisitiza kuwa hazina manufaa kwa wananchi wa Jimbo la Buchosa.
Akizungumza wakati wa mkutano huo wa kampeni, Katalyeba amesema wananchi wa Buchosa “wameshatosheka na kasi ya maendeleo” chini ya uongozi wa Rais Samia na Mbunge Shigongo, hivyo kuomba washirikiane kuhakikisha ushindi wa Chama Cha Mapinduzi unaendelezwa katika uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.