Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
"Ajenda ya Katiba mpya sio ajenda ya wapinzani, ni ajenda ya Chama cha Mapinduzi kuanzia Awamu ya Nne ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Awamu ya Sita ya Samia Suluhu Hassan. Na tayari ameweka kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi, alishatoa ahadi, na tayari mchakato umeshaanza na unaendelea. Kwa hiyo sio ajenda ya wapinzani. Wapigieni makofi sana kwa aibu, makofi hayo yawafikie kwa aibu... ni makofi ya aibu."
"Kwa hiyo ajenda hii sio mpya, wala jambo la kusema kwamba Katiba mpya... Mtakumbuka katika Awamu ya Nne ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa nia njema serikali itenga fedha, ikatenga fedha, wabunge maalum wakateuliwa."
Ameyasema hayo Kijiji cha Kangagani, Kaskazini Pemba wakati akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuweka Jiwe la Msingi la Skuli ya Amali inayojengwa kwa Shilingi Bilioni 4.