Mojawapo ya Jukumu la Wizara ya Kazi na Ajira ni kuhakikisha kunakuwa na Mazingira wezeshi ya Ajira kwa wote wenye sifa za Ajira,haki na wajibu wa mfanyakazi.
Kwa kuanzia Mh. Naibu Waziri angelisaidia mchakato wa kurasimisha baadhi ya Ajira zisizo rasmi zinazoajiri vijana wengi ili waweze kupata Mikopo ya kujikwamua, kuajili wengine na kukuza mitaji mfano.. Kazi zote za ufundi na viwanda vidogox2.
Mh. Naibu Waziri tunaomba ufanye utafiti wa tatizo la Ajira ili utape uhakika wa hali halisi mtaani,vijana wengi wanahitaji msaada wa elimu ya ujasiriamali,utunzaji wa fedha na namna ya kuanzisha na kukuza mitaji mikubwa ya biashara.
Kama Wizara andaeni semina,warsha,makongamo na watembeleeni Vijana sehemu za kazi ili mpate kutatua changamoto zinawakabili.