Akabi kemanya
JF-Expert Member
- Oct 26, 2021
- 226
- 346
Usimlaumu Katambi kwani juzi kati Samia alisema Nini kuhusu vijana na ajira?Naibu Waziri anayehusika na mambo ya Ajira sijui na Nini vile, amejitokeza na kuwalaumu vijana wenzake kuwa ni walalamishi na wanachagua Ajira! Sina tatizo na Hilo ila tatizo langu ni wapi zilipo Ajira ambazo vijana walipewa wakazigomea?
Ni ujinga na kujilisha upepo kuona au kuwadharau vijana ambao Leo hii yeye akiondoshwa hapo hatakua na Cha kufanya.
Kuna PhD holder alikua RC Morogoro, alivyotumbuliwa akaanza kulalamika kuwa family nzima inategemea yeye! Sasa huyo ni PhD holder, je hali ikoje kwa vijana? Ni kweli tuna vijana wavivu?
Kuna vijana walikua wanashinda ONLINE wanafanya kazi mbalimbali ONLINE na walikua wanalipwa vizuri tu, akatokea Mpuuzi huko huko CCM akasema hakuna kufanya malipo kwa PayPal sijui na Nini Ile. Vijana wengi Ajira zikafa.
Hawajapona vizuri akatokea kichaa mwingine akaongeza Bei ya bundle kwa 50%. Yaani wakati ulimwengu unapunguza gharama za bundle Tanzania wanaongeza gharama Kisha anatokea mwendawazimu mmoja anawalaumu vijana. Dah!
Ombacradhi na wewenataka kuungana na Naibu Waziri kuna baadhi ya vijana wana hiyo kasumba
nataka kuungana na Naibu Waziri kuna baadhi ya vijana wana hiyo kasumba
Huyu jamaa nilikuwa namkubali sana kipindi tupo chuo shycom kampeni za uchaguzi mkuu ubunge Kati masele(ccm) vs marehemu shelembi (chadema),ila sasa nimeamini hakuna mkate mgumu mbele ya chair,amekuwa mtu wa kutukejeli vijana kuhusu ajira kweli? Aaa 2025 hatoboi kabisa ndani tu ya ccm humohumo,ovyo kweli,si ageongea mengine tu nasi kutukejeli ase!Naibu Waziri anayehusika na mambo ya Ajira sijui na Nini vile, amejitokeza na kuwalaumu vijana wenzake kuwa ni walalamishi na wanachagua Ajira! Sina tatizo na Hilo ila tatizo langu ni wapi zilipo Ajira ambazo vijana walipewa wakazigomea?
Ni ujinga na kujilisha upepo kuona au kuwadharau vijana ambao Leo hii yeye akiondoshwa hapo hatakua na Cha kufanya.
Kuna PhD holder alikua RC Morogoro, alivyotumbuliwa akaanza kulalamika kuwa family nzima inategemea yeye! Sasa huyo ni PhD holder, je hali ikoje kwa vijana? Ni kweli tuna vijana wavivu?
Kuna vijana walikua wanashinda ONLINE wanafanya kazi mbalimbali ONLINE na walikua wanalipwa vizuri tu, akatokea Mpuuzi huko huko CCM akasema hakuna kufanya malipo kwa PayPal sijui na Nini Ile. Vijana wengi Ajira zikafa.
Hawajapona vizuri akatokea kichaa mwingine akaongeza Bei ya bundle kwa 50%. Yaani wakati ulimwengu unapunguza gharama za bundle Tanzania wanaongeza gharama Kisha anatokea mwendawazimu mmoja anawalaumu vijana. Dah!
Ukiwa CCM akili unaacha njeKwa nafasi yake anapaswa kuja na mikakati kamambe ya namna gani atawakwamua vijana wenzake na ukosefu wa ajira na sio tofauti na hivyo.
Akikujibu nambieWale ambao hawana hiyo kasumba wamepata hizo ajira wakagoma?
Makini my foot 🦶Kama ni kweli kasema hii maneno
Naamini wenye Chama Chao na serikali hawatavumilia hii choko choko
CCM ni Chama cha watu makini
Yeye hayamhusu hayoMojawapo ya Jukumu la Wizara ya Kazi na Ajira ni kuhakikisha kunakuwa na Mazingira wezeshi ya Ajira kwa wote wenye sifa za Ajira,haki na wajibu wa mfanyakazi.
Kwa kuanzia Mh. Naibu Waziri angelisaidia mchakato wa kurasimisha baadhi ya Ajira zisizo rasmi zinazoajiri vijana wengi ili waweze kupata Mikopo ya kujikwamua, kuajili wengine na kukuza mitaji mfano.. Kazi zote za ufundi na viwanda vidogox2.
Mh. Naibu Waziri tunaomba ufanye utafiti wa tatizo la Ajira ili utape uhakika wa hali halisi mtaani,vijana wengi wanahitaji msaada wa elimu ya ujasiriamali,utunzaji wa fedha na namna ya kuanzisha na kukuza mitaji mikubwa ya biashara.
Kama Wizara andaeni semina,warsha,makongamo na watembeleeni Vijana sehemu za kazi ili mpate kutatua changamoto zinawakabili.