Katambi: Madaraka ni dhamana, si leseni ya kupuuza haki, ukweli na uwajibikaji

Katambi: Madaraka ni dhamana, si leseni ya kupuuza haki, ukweli na uwajibikaji

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa wito kwa viongozi wa dini na jumuiya za kiraia nchini kuchagua njia ya maridhiano, kufuata sheria na kulinda amani ya taifa, akionya kuwa machafuko na vurugu huumiza wananchi wasio na hatia na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Katambi ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2026, alipokuwa akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya usajili wa jumuiya za kiraia nchini Tanzania.

"Nchi yetu iliingia katika madhila ya changamoto zilizojitokeza na vurugu mbalimbali ambazo zilipelekea kupatikana kwa changamoto aidha watu kupoteza maisha ama kujeruhika ama uharibifu wa mali za serikali na za watu binafsi. Lakini hii yote ilitokana na baadhi yetu kuchagua kuamini katika vita, machafuko na vurugu kuliko maridhiano. Kuamini katika njia ya kutafuta maslahi fulani au madaraka kwa njia isiyokuwa ya kikatiba au ya kisheria...

Soma Pia: Katambi: Uhuru na demokrasia bila mipaka ni fujo, tusifiche uhalifu kwenye siasa

Waheshimiwa viongozi wa dini, viongozi wa jumuiya, haya yote ni sisi Watanzania kuyatafakari. Hivi kweli tunapenda vita? Hivi kweli tunapenda machafuko? Na je tuko tayari na tumejiuliza nani atabaki salama?", amehoji Katambi.

Ameongeza kuwa pindi sheria na haki zisipofuatwa, makundi yaliyo hatarini kama vile wazee, wanawake, na watoto ndio wanaoteseka zaidi kwasababu hawawezi kukimbia pindi machafuko yanapotokea.
 
Wao wamechukua hatua gani ili kuzuia hayo machafuko? Maana kabla ya uchaguzi watu waliomba wakae meza moja wabadili katiba na sheria za uchaguzi wao serikali wakajifanya wajeuri leo tumefika hapa wanaanza ngonjera hebu wasituchoshe bwana.Sisi wananchi kwa kweli tumechoka sana na maneno yenu.
 
"Lakini hii yote ilitokana na baadhi yetu kuchagua kuamini katika vita, machafuko na vurugu kuliko maridhiano. Kuamini katika njia ya kutafuta maslahi fulani au madaraka kwa njia isiyokuwa ya kikatiba au ya kisheria..."
 
Hawa jamaa nimewachunguza kwanini kila wakiweka neno "haki" lazima lifuatie neno "uwajibikaji".

Nikagundua kwao wakisema "uwajibikaji" wanamaanisha kutii uminywaji wa haki wanaodai kuihubiri.

Wanataka wakituteka tutulie chini kimya, wakitupoteza tutulie kimya, huo kwao ndio uwajibikaji!
 
Back
Top Bottom