Katambi: Tuwatie moyo askari, tusiwatweze na kuwaumiza wamejitoa maisha yao

Katambi: Tuwatie moyo askari, tusiwatweze na kuwaumiza wamejitoa maisha yao

Lazima uwe kundi la ibilisi kuwatia moyo wauaji. Kuwatia moyo maana yake ni kuwahamasisha waendelee kuua zaidi na kuteka zaidi, bila ya kujua kuwa siku nyingine watakuua na wewe mwenyewe, ndugu zako au wanafamilia wako. Polisi wa Tanzania wa sasa ni laana kwa mwanadamu. Ni aheri hata tungekuwa na sungusungu kuliko hawa wauaji.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema kuwa amani iliyopo nchini kwa kiasi kikubwa imechangiwa na kazi kubwa inayofanywa na majeshi ya ulinzi na usalama, huku akitoa wito kwa wananchi kutotoa kauli mbaya na kutowatweza askari na badala yake wawatie moyo kwani wamejitolea maisha yao kwaajili ya kulinda raia na mali zao.

Soma Pia: Katambi: Wizara kupitia Jeshi la Polisi imepokea Tsh. Bilioni 247.48 kwa ajili ya ununuzi wa magari 412 na pikipiki 29 za kuongozea misafara

Katambi ameyasema hayo leo Mei 25, 2026, wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka 2026/2027, Bungeni jijini Dodoma.

Naunga mkono hii hoja, hata humu niliwahi kushauri Jeshi la polisi likifanya vyema, lipongezwe, hongera FFU kusambaratisha maandamano bila virungu, mabomu ya machozi, risasi za moto, bila maafa!

Pia nikawasisitiza polisi wetu Ombi kwa Polisi: Nyinyi ni wenzetu, kwenye Maandamano yetu tafadhali msigeuke Gestapo au Makaburu!

Na kutumia affirmative action ya kuwataja polisi in a good way Pongezi Jeshi la Polisi. Japo Nabii hakubaliki nyumbani, Jeshi sasa ni Sikivu, Most friendly na very hospitable
Kutumia majina mazuri kwa jeshi letu la polisi kama jeshi letu safi la polisi IGP Kamanda Sirro, Usiruhusu Vifo Vya Uzembe Kama Huu Kuchafua Jeshi Letu Safi la Polisi!.

P
 
Back
Top Bottom