Katarama Buses: Route ya Kampala-Ben, na Ben-Kisangani itaanza karibuni

Katarama Buses: Route ya Kampala-Ben, na Ben-Kisangani itaanza karibuni

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Kweli wapambe wa tajiri wana nguvu.

Tayari wapambe walishaenda kampala na kisanganj kuangalia njia na kushughulikia vibali, japo wengine wana mshauri center iwe Kampala to Juba na Kampala to Ben, huku wakimweleza kisangani aende baadae.

Mmiliki wa mabasi ya Classic nae anachekelea apate Mtanzania mwenzie huko ili wapambane ni full vurugu,
Lakini ndio biashara ikikataa upande mmoja basi unajiongeza upande mwingine, hauwezi ukakaa bila kazi wakati dunia ni kijiji na kote fursa zipo.

Kila la kheri Katarama,

FB_IMG_17263964550191126.jpg
 
Zaburi 109
BHN

Zaburi 109​

Lalamiko la mtu taabuni
(Kwa Mwimbishaji. Wimbo wa Daudi)
1Usinyamaze, ee Mungu ninayekusifu!
2Watu waovu na wadanganyifu wanishambulia,
wanasema uongo dhidi yangu.
3Wanasema maovu juu yangu,
na kunishambulia bila kisa.
4Ingawa niliwapenda, walinishtaki,
hata hivyo niliwaombea dua.
5Wananilipa uovu kwa wema wangu,
na chuki kwa mapendo yangu.
6Umweke hakimu mbaya dhidi ya adui yangu;
na mshtaki wake ampeleke mahakamani.
7Anapohukumiwa apatikane na hatia;
lalamiko lake lihesabiwe kuwa kosa jingine.
8 Siku za maisha yake ziwe chache,
mtu mwingine na achukue kazi yake!
9Watoto wake wawe yatima,
na mke wake awe mjane!
10Watoto wake watangetange na kuombaomba;
wafukuzwe katika magofu ya nyumba zao!
11Anayemdai kitu amnyanganye mali yake yote;
na wageni wanyakue mapato ya jasho lake!
12Pasiwe na mtu wa kumwonea huruma,
au Kuwatunza watoto wake yatima!
13Wazawa wake wote wafe;
jina lake lisahauliwe katika kizazi kijacho!
14Mwenyezi-Mungu aukumbuke uovu wa wazee wake,
dhambi za mama yake zisifutwe kamwe!
15Mwenyezi-Mungu azikumbuke dhambi zao daima;
lakini wao wenyewe wasahauliwe duniani.
16Mwovu huyo hakujali kabisa kuwa na huruma,
ila aliwadhulumu maskini na fukara,
kadhalika na watu wanyonge mpaka kifo.
17Yeye alipenda kulaani watu,
laana na impate yeye mwenyewe.
Hakuwatakia wengine baraka,
basi, asipate baraka yeye mwenyewe.
18Kwake kulaani ni kama kuvaa nguo,
basi, laana hizo zimloweshe kama maji,
zimwingie mifupani mwake kama mafuta.
19Laana zimfunike kama nguo,
zimzunguke daima kama ukanda.
20Mwenyezi-Mungu awalipe hayo hao watu wanaonishtaki,
naam hao wanaosema mabaya dhidi yangu.
21Lakini ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wangu,
unitendee kadiri ya hisani yako;
uniokoe, kwa sababu ya wema wa fadhili zako!
22Mimi ni maskini na fukara;
nimejeruhiwa mpaka moyoni mwangu.
23Natoweka kama kivuli cha jioni;
nimepeperushwa kama nzige.
24Magoti yangu yamenyongonyea kwa mfungo;
nimebaki mifupa na ngozi.
25 Nimekuwa dhihaka tupu kwa watu;
wanionapo hutikisa vichwa vyao kwa dharau.
26Unisaidie, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu;
uniokoe kadiri ya fadhili zako.
27Waoneshe watu kuwa ndiwe uliyetenda hayo,
wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ndiwe uliyefanya hivyo.
28Waache walaani, lakini wewe unibariki;
wanaonishambulia waaibike, nami mtumishi wako nifurahi.
 
Mama Samia njoo vuna kura zetu huku kanda ya ziwa kwa kutetea weusi wenzako Katarama kwenye hii biashara against waarabu Ally's, hawa wanaotaka kujiona Miungu watu wakati baba zao walikuja Tanzania kwa kutumia upepo wa Mansoon wind na sasa wanajibebea mali tu watakavyo. Yaani inashangaza Ally's na Katarama zinatoka Dar muda mmoja halafu Ally's inawahi kufika huku Katarqma anadakwa kachezea VTS alafu Ally's ndio kwanza anaongezewa route za kwenda! LATRA mnatuona watanzania mapoyoyo kutokujua huu ni mchezo mchafu ?
 
Jamaa kaja kuleta ushindani wa bus mpya na nzuri serekali inamfungia biashara na hana record zozote za ajali alafu Allys ambae kila mara wanapata ajali wao hawaguswi hivyo ndo viashiria vya uwepo wa rushwa.

Bahati nzuri katarama anabiashara nyingi tu huku kwenye mabus ni kama alileta burudani acha aondoe bus zake atuache na vibuyu vya Golden dragon maana sisi wa Tz hatujui vitu vizuri mtu akileta ushindani wa kimaendeleo tunamchukia
 
Mama Samia njoo vuna kura zetu huku kanda ya ziwa kwa kutetea weusi wenzako Katarama kwenye hii biashara against waarabu Ally's, hawa wanaotaka kujiona Miungu watu wakati baba zao walikuja Tanzania kwa kutumia upepo wa Mansoon wind na sasa wanajibebea mali tu watakavyo. Yaani inashangaza Ally's na Katarama zinatoka Dar muda mmoja halafu Ally's inawahi kufika huku Katarqma anadakwa kachezea VTS alafu Ally's ndio kwanza anaongezewa route za kwenda! LATRA mnatuona watanzania mapoyoyo kutokujua huu ni mchezo mchafu ?
Tafuta hela wewee
 
M
Kweli wapambe wa tajiri wana nguvu.

Tayari wapambe walishaenda kampala na kisanganj kuangalia njia na kushughulikia vibali, japo wengine wana mshauri center iwe Kampala to Juba na Kampala to Ben, huku wakimweleza kisangani aende baadae.

Mmiliki wa mabasi ya Classic nae anachekelea apate Mtanzania mwenzie huko ili wapambane ni full vurugu,
Lakini ndio biashara ikikataa upande mmoja basi unajiongeza upande mwingine, hauwezi ukakaa bila kazi wakati dunia ni kijiji na kote fursa zipo.

Kila la kheri Katarama,

View attachment 3098052
Mama anafungua nchi!!🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom