Katarama Buses: Route ya Kampala-Ben, na Ben-Kisangani itaanza karibuni

Kuliko kumfungia mtu biashara, bora apigwe faini alipe au basi husika pekee ndo lifungwe
 
Tatizo kampuni nyingi za mabasi na malori viongozi wenye mamlaka wana ya kwao humo ndio hao wanaoharibia watu wasio viongozi, mabasi ya Katarama yalikuwa yamepandisha hadhi hata ya nchi Ktk medani za usafiri wa abiria
 
Hii kitu imenishangaza sana, kwanini Katarama kafutiwa leseni ya Usiku

Je ni kweli au ndio figisu za bongo

Dah Team Scania ni pigo kubwa

Acha tu tukapande michina maana hakuna namna
 

Kila mara maafisa wa serikali utengeneza mazingira magumu kwa wafanya biashara, sasa hii ndo nini? Raia ndo tunateseka wakati wao wanatumia V8 kusafiri mikoani. Sijuhi hawa jamaa wasaidiweje?
 
Habari njema sana hii. Tulikuwa tunapata shida sana kusafiri kwenda Beni. Uingie Mbarara, upite mpondwe, ofcourse ndiyo barabara hiyohiyo tatizo ni hakuna reliable transport na hapo bado haujahisiwa kuwa wewe ni Mwanajeshi au Jasusi.
Angalau sasa kutakua kuna usafiri rasmi badala ya usafiri kafiri uliopo
 
Wangemuacha wangepaki mikokoteni yao io, Angalia sasa chuma kali izo zinaenda uganda mweee!!!!!
 
Maisha popote chezea pua ila sio biashara za watu, Tanzania watu wenye dhamana ya taasisi na idara za Serikali wamejaa wivu na ni wachawi
Sisi wabongo hata ambao hawako kwenye mfumo, leta wivu sana. Kuna mtu anaweza kukusagia Kunguni mpaka ukashangaa. Unakuta hamna uhusiano wa biashara zenu au issue zenu lkn anakusagia kunguni balaaa
 
Unamnyan'ganya mtu leseni badala ya kumuonya. Wtz wanakosa ajira.

Makosa ya magari ni maonyo na fine kubwa ukitaka lkn sio kuzuia mtu asifanye biashara. Unamnyima haki yake ya kikatiba kufanya kazi na kupata kipato eboo
Halafu unawakuta na kodi wanataka haswaa
 
Hivi ndugu yangu unajua kuwa serikali inampa Ruzuku Bakhresa, Mo Dewji, Murzah na Rostam. Tanzania hadi tutoboe bado sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…