MARIO PONSIANO MTUNGE
New Member
- Jun 5, 2023
- 1
- 2
Ilikuwa ni siku yenye mawingu mepesi sana na sauti za ndege zilikuwa zikisikika kutoka katika viunga vya chuo ambacho Katarina alikuwa akisoma.
Siku hiyo ilikuwa ndiyo siku ambayo wanachuo wengi akiwemo Katarina, walikuwa wakimalizia mitihani yao. Katarina na wanachuo wenzake walikuwa wakisoma kwenye vimbweta kwa njia ya majadiliano.
Muda wa kufanya mtihani ulifika, Katarina alisali kuomba msaada wa Mungu kisha akajiweka tayari kupokea karatasi za kujibia. Wakati ugawaji wa karatasi za kujibia ukiendelea, Katarina alisahau kuhifadhi simu yake kwenye mkoba wake na hivyo alibaki nayo kwenye mfuko wa gauni lake na akaingia nayo kwenye chumba cha mtihani. Mjomba wake hakujua kama Katarina yupo katika mfululizo wa mitihani ya chuo, hivyo alimpigia simu.
Mwalimu wa somo lile aliyefahamika kwa jina la Dkt. Pius ambaye alikuwa miongoni mwa wasimamizi wa mtihani ule, aliamuru Katarina arudi nyumbani.
Wengi hawakujua sababu ya yote lakini kabla hawajaingia chumba cha mtihani Katarina alikuwa amearifiwa na ndugu zake arudi nyumbani kwani kulikuwa na jambo la dharula. Ingawa bado walimficha lakini walikosa namna ya kumweleza kuhusu kifo cha mama yake na kaka yake Zakaria ambao walikufa kwa ajali ya bodaboda.
Katarina alirudi nyumbani kushiriki mazishi na baada ya siku chache za mazishi, Katarina alikuwa amesharejea chuoni. Akiwa kitandani akitafakari msiba uliomkubwa alikua pia anawaza hatima yake kitaaluma. Punde alipokea ujumbe kutoka kwa Dkt Pius aliyekuwa akihitaji kuonana naye siku ya jumapili.
Jumapili ilifika na wakati wa mchana, Dkt. Pius alikuwa akijisemea akilini mwake “haka katoto nimemnasa kwenye kumi na nane zangu!! akiwa mwaka wa kwanza alinikataa lakini safari hii hatoboi lazima anase.” Katarina alifika hotelini na alielekezwa na dada wa mapokezi kuelekea upande wa mashariki ambako ndiko alikokuwa ameketi Dkt. Pius karibu na kiunga chenye mti wa mwarobaini.
Dkt Pius alikuwa ameagiza nyama choma pamoja na soda. Ingawa Katarina alitaka kukataa, alikumbuka maneno ya wahenga wasemayo “usikatae akupacho mswahili kwa ridhaa yake lakini usikubali akudai malipo yake”. Katarina aliitafuna ile nyama lakini mwisho alitambua dalili mbaya hivyo alimwandikia rafiki yake Naomi ujumbe wa kuomba amtumie ujumbe usemao “Katarina rudi nyumbani moto unaunguza mali zetu” hiyo ndiyo ilikuwa ponapona ya Katarina hivyo alimwacha Dkt Pius palepale akipiga miayo isiyotokana na njaa.
Kisheria Katarina alipaswa kurudia mtihani ule na aliweza kuufanya pasipo tabu yoyote na baada ya siku chache matokeo ya mtihani yalitoka na kama kawaida Katarina alifungua mtandao wake wa taarifa za chuo kutazama matokeo yake. Alifurahi tena kuona amefaulu katika masomo yote tisa ya muhula ule. Akiwa kapata GPA ya 4.4, Katarina alikuwa na ‘A’ nane, na ‘C’ moja katika somo la Dkt Pius na inasadikika Katarina alifanya vizuri mtihani wa marudio na hakuwekewa alama sahihi kutokana na hasira ya Dkt Pius.
Orodha ya wahitimu ilitolewa, Katarina naye alipaswa kufanya mahafali. Mara nyingi kukiwa na mahafali ya chuo wahitimu wengi hupenda kufanya tafrija zao sehemu mbalimbali za mji. Katarina aliandaa keki yake na baada ya mashangilio ya pamoja alichukua keki yake kisha akaenda nayo mjini. Alipofika mjini alianza kuwatembelea vilema na wahitaji waliokuwa pembezoni mwa barabara wakiomba msaada. Aliwalisha vipande vya keki ile hadi vikaisha na kuwapatia kila mmoja kiasi cha shilingi 500.
Kwa kuwa alionekana akisherekea mahafali kwa namna ya tofauti, Katarina alinaswa na kamera za kituo fulani cha televisheni. aliulizwa kama jambo analolifanya lina tija yoyote, Katarina alijibu akisema “nimependa kufurahi kwa namna hii, nilipokuwa nasoma nilihitaji sana msaada na niliona mimi pekee ndiye nahitaji kusaidiwa, mara nyingi nilisahau kama kuna wahitaji zaidi yangu, tena kwa kuwa sikuwa na chochote cha kuwapa hawa kila nilipopita hapa nilikosa amani tena waliponiomba niliwapita kama siwaoni lakini leo pia sina cha kuwapa hawa hivyo nimekuja nifurahi na hawa wenzangu” Mwandishi akamuuliza tena akisema “sasa unafikiri leo tu itatosha kwa mhitaji huyu kuridhika na ukarimu wako?” Katarina aliinamisha kichwa chake akamtazama yule kilema aliyekuwa karibu naye kisha akamjibu mwandishi akisema “kilema huyu anahitaji watu 365 tu!! kwa mwaka ili aweze kuwa na furaha. hata hivyo Katarina alikataa kupigwa picha kwasababu anaamini kwamba ukitoa au ukipokea chochote kwa hiari na kwa roho safi si lazima utangaze wala utangazwe.
Siku si nyingi Katarina alibahatika kupata kazi ya uwakala katika shirika la kimataifa la kuwainua vijana na alifanya kazi hiyo kwa muda wa miaka 13 akiwa mjumbe wa chini katika ngazi ya wilaya na alipomaliza kazi hiyo alishawishika kuanzisha kikundi cha vijana alichokiita (VINAMA) yaani “Vijana Na Maendeleo”, alishughulika na vijana hata akateuliwa kuwa waziri wa vijana ambapo alifanya kazi hiyo hadi alipostaafu kwa hiyari akiwa namiaka 58.
Siku moja katika uzee wake Bi Katarina alipata mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la vijana kitaifa.
Katika hotuba yake alisema.
“Waheshimiwa vijana, wageni waalikwa wa kitaifa na kimataifa, viongozi wa serikali na dini, taasisi mbalimbali za vijana na makundi mbalimbali, na watu wote mliokusanyika hapa nathamini sana uwepo wenu .
Ndugu zangu napenda kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kutuweka hai hata akaruhusu tukusanyike pamoja siku ya leo.
Ndugu zangu nafikiri mnafahamu kwamba nimesema sana nanyi katika matamasha mbalimbali hivyo leo nitasema kwa ufupi mambo matatu tu muhimu.
Ndugu zangu vijana; Naomba zingatieni sana umoja kwasababu sisi wazee wenu hatukuweza kufika tulipopataka kwasababu tulipuuza mshikamano tukautukuza ubinafsi.
Wapendwa wanangu; kuna mali adhimu zinaitwa Uhuru, Umoja na Amani naomba mali hizo bandikeni kwenye mishipa ya mioyo yenu.
Na Mwisho wapendwa vijana wangu nimependa shauku yenu katika siasa ila mkiwa huko msikubali kutumika kushangilia au kutetea kila jambo hata ambalo halina tija kwa taifa lenu, tambueni kwamba kuunga mkono kila jambo hata lisilofaa si adabu ya kisiasa na kupinga kila jambo hata la msingi si kipimo cha kuwa mwanaharakati bora.
Bi Katarina ni mzee sasa wa miaka 89. Yeye anayo mengi ya kuyakumbuka lakini akili yake imechoka. Ameonja matunda mengi ya mshikamano tena si tu katika nchi yake bali kimataifa pia. Uso wake uliokunjamana hauwezi kuonesha kama anatabasamu lakini furaha yake moyoni ni namna ambavyo anaona watu wa makundi yote pamoja na vijana wengi wakionesha nia za kulifaa Taifa na kuipokea kwa mikono miwili kampeni ya vijana na maendeleo ambayo yeye anaona bado haijapewa kipaumbele kama inavyostahili.

Upvote
2