Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amesitisha huduma zote za usafiri katika Barabara ya Sitalike kuelekea KIZI Mkoani Rukwa na badala yake itumike Barabara ya Kibaoni Sitalike.
Agizo hilo limetolewa mara baada ya abiria kukwama katika Mto Sitalike ambapo daraja limefurika maji huku abiria hao wakikwama zaidi ya Saa 15.
Aidha, Mrindoko amepiga marufuku kwa mtu yeyote kupita kwenye maji wakati mto umejaa mafuriko.