Katavi: Barabara imefungwa baada ya mafuriko kukwamisha Abiria

Katavi: Barabara imefungwa baada ya mafuriko kukwamisha Abiria

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607


Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amesitisha huduma zote za usafiri katika Barabara ya Sitalike kuelekea KIZI Mkoani Rukwa na badala yake itumike Barabara ya Kibaoni Sitalike.

Agizo hilo limetolewa mara baada ya abiria kukwama katika Mto Sitalike ambapo daraja limefurika maji huku abiria hao wakikwama zaidi ya Saa 15.

Aidha, Mrindoko amepiga marufuku kwa mtu yeyote kupita kwenye maji wakati mto umejaa mafuriko.

Hali ilivyo baada ya maboresho - Katavi: Barabara iliyofungwa kutokana na athari za mafuriko kuanza kutumika
 
Bado hata daraja la mto MNYAMAZI kati ya Uvinza na Mpanda nalo lilifurika maji for 3days hadi wakati mie naahirisha safari.
 
Back
Top Bottom