Katavi kuunganisha nguvu kuleta usawa wa kijinsia siku ya maadhimisho ya wanawake Duniani

Katavi kuunganisha nguvu kuleta usawa wa kijinsia siku ya maadhimisho ya wanawake Duniani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mkoa wa Katavi hii leo umezindua maadhimisho ya siku ya Wanawake ambayo ulimwenguni yatahitimishwa March 8, 2025 huku yakiangazia nyanja kuanzia mafanikio, changamoto na hata mustakabali wao, sio tu kwa wanawake bali pia wasichana.

Kote mkoani humo, Taasisi za serikali na zisizo za serikali wanaungana na wanawake hii leo kuanza kuadhimisha siku hiyo, kwa kuwasilisha madai yao na kujadiliana kwa kina namna watakavyojikwamua kutoka kwenye vizingiti na vikwazo vinavyozuia kushamiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu, ameweka wazi kuwa maadhimisho hayo kimkoa yatafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili manispaa ya Mpanda huku akiomba wananchi kushiriki kwa wingi.
WhatsApp Image 2025-02-28 at 17.28.58_ef77579e.jpg

WhatsApp Image 2025-02-28 at 17.24.32_f1f7527f.jpg

WhatsApp Image 2025-02-28 at 17.25.23_80416b6a.jpg
Akizundua maadhimisho hayo, Buswelu amesema uamuzi wa Umoja wa Mataifa wa kuanzisha siku ya wanawake Duniani unatokana na ukweli kwamba masuala ya haki, Maendeleo na Usawa wa jinsia yanahitaji msukumo maalumu na wa kipekee kutoka jamii husika.

Kiongozi huyo akiwa katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa, amefafanua kuwa Tanzania imejiwekea utaratibu wa kutekeleza maadhimisho katika ngazi ya Mikoa kila baada ya miaka 5 ambapo lengo ni kutathimini utekelezaji wa Ajenda ya usawa wa kijinsia, Haki na Uwezeshaji wa Wanawake katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

Buswelu ameeleza kuwa katika mkoa huo, Maadhimisho hayo yataambana na shughuli mbalimbali ambapo baadhi ya shughughuli hizo ni kufanya kongamano la wanawake , kuwatembelea watoto walio kwenye mazingira magumu na kuwafanyia matendo ya huruma na kutembelea mradi wa machinga.

Mkurugenzi wa Kampeni ya Mwanamke Jasiri, Zefrine Machesha ameeleza kuwa kupitia ziara ya Rais Dkt Samia Suluhu aliyoifanya mwaka 2024 baada ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Katavi asilisikitishwa kuona watoto wadogo wakijifungua jambo ambalo waliamua kuanzisha kampeni hiyo ya kupiga mimba na ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia.
WhatsApp Image 2025-02-28 at 17.26.03_2ed47fcf.jpg
Machesha amesema lengo la kampeni ya Mwanamke Jasiri ni kuhakikisha mwanamke wa mkoa huo anaweza kujisimamia mwenyewe kuanzia ngazi ya familia ili kupata uwezo wa kupambana.

“Kampeni hii ya Mwanamke Jasiri leo hii imeambatana na kufanya matembezi ya amani kuwaonesha wanawake wa mkoa wa Katavi kwamba tuko sawa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni na kutoa hamasa kwa mwanamke kuwa na fikra chanya kwamba akisema anaweza kufanya basi anaweza kufanya jambo lake” anasema.

Mariam Hussan, Mkazi wa mtaa wa Misukumilo manispaa wa Mpanda akiwa kwenye matembezi ya amani katika kampeni ya Mwanamke Jasiri amesema kuwa wakati serikali ikiendelea na juhudi za kupigania usawa lakini bado hakuna usawa wa kijisia na sasa wanaitumia fursa hilo kulimulika suala hilo kwa mtizamo wa kijinsia.

Aidha amegusia suala la pengo lililopo kwenye malipo kati ya wanaume na wanawake katika kazi za sekta binafsi na kusema hata hayo yanapaswa kuzingatiwa kwa watuga sheria na sera ili kuondosha tatizo hilo.

Maadhimisho ya mwanamke Duniani yanabeba kauli mbiu ya mwaka huu ni wanawake na wasichana 2025 tuimarishe haki usawa na uwezeshaji.
 
Back
Top Bottom