Katavi: Mganga alawiti watoto sita akiwapa matibabu

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Mganga wa kienyeji mkazi wa Majengo ya Mpanda mkoani Katavi, Akili Abakuki maarufu kama Jimmy (38) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwalawiti watoto sita wakati akiwapatia matibabu nyumbani kwake.

Kaimu wa Jeshi la Polisi Mkoani hapo, Sylivester Ibrahim amesema mtuhumiwa alikamatwa Mei 8 mwaka huu baada ya mmoja wa wazazi wa watoto hao kugundua kuwa mwanaye mwenye umri wa miaka 10 aliyepelekwa kwa mganga huyo kutibiwa amelawitiwa.

Kamanda amebainisha kuwa, wazazi wa watoto hao wenye umri kati ya miaka 6 na 12 waliwapeleka kwa mganga huyo ambapo aliwapa masharti kuwa, tiba zake ni lazima azitoe usiku hivyo lazima watoto hao walale nyumbani kwake bila ya wazazi wao.

Inadaiwa usiku mganga huyo huwarubuni kwa zawadi ndogo ndogo kama biskuti na peremende kisha kuwapaka mafuta mwili mzima na kuwaingilia kimwili.

Anasema vitendo hivyo huvifanya chumbani kwake usiku wa manane huku akiwatishia watoto hao kutowaambia wazazi wao kitendo walichofanyiwa.

Kamanda anawasihi wazazi kufuatilia vitendo wanavyoweza kuwa wamefanyiwa watoto wao na kuwahimiza waache kushikilia imani potofu za kishirikina.
 
UJINGA NI MTAJI MKUBWA KWA:
1.WAGANGA WA JIENYEJI
2.MITUME & MANABII
3.WANASIASA

MGANGA ALITAKIWA KULAWITI WAZAZI KWA NIABA YA WATOTO, SASA ANA KESI YA KUJIBU
 
Ukifika gerezani ukisimulia kesi eti nimelawiti mtoto, nyapara malizana nae shenzi kbs
 
Kunyonga tu hapa hamna haki za binadamu wal feminist shenzi kama huyp kumaliza tu kafanya mashoga hao watoto
 
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi, linamshikilia mganga wa kienyeji, Akili Abakuki, maarufu Jimmy (38), mkazi wa Majengo, Manispaa ya Mpanda kwa tuhuma za kuwalawiti watoto sita nyakati za usiku alipokuwa akiwapatia matibabu ya tiba za asili.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Sylvester Ibrahim, alisema juzi mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 8, majira ya saa 7:00 mchana katika eneo la Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Katavi, mjini hapa.

Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya mama mmoja kugundua mtoto wake wa miaka 10, mwanafunzi wa darasa la tatu (jina limehifadhiwa) aliyekuwa amempeleka kwa mganga huyo kupatiwa matibabu ya asili, amelawatiwa.

Kamanda wa Ibrahim alisema baada ya kupatikana taarifa hizo, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa amewalawiti watoto wengine watano wakati akiwafanyia matibabu. Watoto hao wanao umri kati ya miaka sita na 12.

Alisema wazazi wa watoto hao walikuwa wakiwapeleka mganga huyo kwa ajili ya kupatiwa tiba za asili na katika tiba hizo. mganga huyo alikuwa akitoa masharti lazima azitoe usiku, hivyo ni lazima watoto hao walale kwake bila wazazi wao kuwapo.

“Ilipokuwa ikifika usiku, mganga huyo alikuwa anawadanganya kwa kuwapatia ndogo kama pipi, biskuti na jojo na kisha anawavua nguo na kuwapaka mafuta mwili mzima na kuwalawiti.

Kamanda Ibrahim alisema vitenzawadi ndogo do hivyo vya kuwalawiti hao alikuwa akivifanya ndani ya chumba chake alichokuwa akiishi watoto huku akiwatishia atawafanyia kitu kibaya iwapo watawaambia wazazi wao kuwa usiku wa manane amewafanyia kitendo hicho.

Kutokana na kuwapo kwa hali hiyo, kamanda amewahimiza wa zazi mkoani Katavi kufuatilia vitendo anmbavyo wanaweza kuwa wamefanyiwa watoto wao na pia wazazi waache tabia ya kuamini imani potofu za kishirikina.
 
Wazazi unamruhusu vip mtot kwenda kulal kwa mganga Tena kjn
 
Hao wazazi ni wajinga.
 
Wazazi unamruhusu vip mtot kwenda kulal kwa mganga Tena kjn
Elimu duni,hii nchi Bado sana,Kuna jamii Bado zinaishi enzi za ujima,hawaamini huduma za kisasa za kitabibu,wanaamini uchawi,kulogwa nk
 
Dqah hafai huyo na wazazi nao wanaachaje watoto kupatiwa tiba peke yao
 
Kwa kweli sijui tunakwenda wapi?
Huu ni ugonjwa ambao hata kuutibu ni vuigumu sana.
Kila kona:
Makazini(ajabu hata wasomi, wanadai "baraka za wazee")
Mashuleni(eti watoto wafaulu mitihani)
Biashara(ndio usiseme)
Kwenye uvuvi(astaghafilulah!)
nk
 
Back
Top Bottom