pye Chang shen
JF-Expert Member
- Jul 11, 2016
- 11,422
- 6,108
Mambo ya kina jimmy hayo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao wazazi kwanza ndio wakuanza nao maana ni wapumbavu na hawana akili.Jeshi la Polisi Mkoani Katavi, linamshikilia mganga wa kienyeji, Akili Abakuki, maarufu Jimmy (38), mkazi wa Majengo, Manispaa ya Mpanda kwa tuhuma za kuwalawiti watoto sita nyakati za usiku alipokuwa akiwapatia matibabu ya tiba za asili.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Sylvester Ibrahim, alisema juzi mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 8, majira ya saa 7:00 mchana katika eneo la Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Katavi, mjini hapa.
Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya mama mmoja kugundua mtoto wake wa miaka 10, mwanafunzi wa darasa la tatu (jina limehifadhiwa) aliyekuwa amempeleka kwa mganga huyo kupatiwa matibabu ya asili, amelawatiwa.
Kamanda wa Ibrahim alisema baada ya kupatikana taarifa hizo, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa amewalawiti watoto wengine watano wakati akiwafanyia matibabu. Watoto hao wanao umri kati ya miaka sita na 12.
Alisema wazazi wa watoto hao walikuwa wakiwapeleka mganga huyo kwa ajili ya kupatiwa tiba za asili na katika tiba hizo. mganga huyo alikuwa akitoa masharti lazima azitoe usiku, hivyo ni lazima watoto hao walale kwake bila wazazi wao kuwapo.
“Ilipokuwa ikifika usiku, mganga huyo alikuwa anawadanganya kwa kuwapatia ndogo kama pipi, biskuti na jojo na kisha anawavua nguo na kuwapaka mafuta mwili mzima na kuwalawiti.
Kamanda Ibrahim alisema vitenzawadi ndogo do hivyo vya kuwalawiti hao alikuwa akivifanya ndani ya chumba chake alichokuwa akiishi watoto huku akiwatishia atawafanyia kitu kibaya iwapo watawaambia wazazi wao kuwa usiku wa manane amewafanyia kitendo hicho.
Kutokana na kuwapo kwa hali hiyo, kamanda amewahimiza wa zazi mkoani Katavi kufuatilia vitendo anmbavyo wanaweza kuwa wamefanyiwa watoto wao na pia wazazi waache tabia ya kuamini imani potofu za kishirikina.
Anawafanya nini vile? Anawapaka mafuta!!!?Mganga wa kienyeji mkazi wa Majengo ya Mpanda mkoani Katavi, Akili Abakuki maarufu kama Jimmy (38) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwalawiti watoto sita wakati akiwapatia matibabu nyumbani kwake.
Kaimu wa Jeshi la Polisi Mkoani hapo, Sylivester Ibrahim amesema mtuhumiwa alikamatwa Mei 8 mwaka huu baada ya mmoja wa wazazi wa watoto hao kugundua kuwa mwanaye mwenye umri wa miaka 10 aliyepelekwa kwa mganga huyo kutibiwa amelawitiwa.
Kamanda amebainisha kuwa, wazazi wa watoto hao wenye umri kati ya miaka 6 na 12 waliwapeleka kwa mganga huyo ambapo aliwapa masharti kuwa, tiba zake ni lazima azitoe usiku hivyo lazima watoto hao walale nyumbani kwake bila ya wazazi wao.
Inadaiwa usiku mganga huyo huwarubuni kwa zawadi ndogo ndogo kama biskuti na peremende kisha kuwapaka mafuta mwili mzima na kuwaingilia kimwili.
Anasema vitendo hivyo huvifanya chumbani kwake usiku wa manane huku akiwatishia watoto hao kutowaambia wazazi wao kitendo walichofanyiwa.
Kamanda anawasihi wazazi kufuatilia vitendo wanavyoweza kuwa wamefanyiwa watoto wao na kuwahimiza waache kushikilia imani potofu za kishirikina.