Jeshi la Polisi Mkoani Katavi, linamshikilia mganga wa kienyeji, Akili Abakuki, maarufu Jimmy (38), mkazi wa Majengo, Manispaa ya Mpanda kwa tuhuma za kuwalawiti watoto sita nyakati za usiku alipokuwa akiwapatia matibabu ya tiba za asili.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Sylvester Ibrahim, alisema juzi mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 8, majira ya saa 7:00 mchana katika eneo la Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Katavi, mjini hapa.
Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya mama mmoja kugundua mtoto wake wa miaka 10, mwanafunzi wa darasa la tatu (jina limehifadhiwa) aliyekuwa amempeleka kwa mganga huyo kupatiwa matibabu ya asili, amelawatiwa.
Kamanda wa Ibrahim alisema baada ya kupatikana taarifa hizo, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa amewalawiti watoto wengine watano wakati akiwafanyia matibabu. Watoto hao wanao umri kati ya miaka sita na 12.
Alisema wazazi wa watoto hao walikuwa wakiwapeleka mganga huyo kwa ajili ya kupatiwa tiba za asili na katika tiba hizo. mganga huyo alikuwa akitoa masharti lazima azitoe usiku, hivyo ni lazima watoto hao walale kwake bila wazazi wao kuwapo.
“Ilipokuwa ikifika usiku, mganga huyo alikuwa anawadanganya kwa kuwapatia ndogo kama pipi, biskuti na jojo na kisha anawavua nguo na kuwapaka mafuta mwili mzima na kuwalawiti.
Kamanda Ibrahim alisema vitenzawadi ndogo do hivyo vya kuwalawiti hao alikuwa akivifanya ndani ya chumba chake alichokuwa akiishi watoto huku akiwatishia atawafanyia kitu kibaya iwapo watawaambia wazazi wao kuwa usiku wa manane amewafanyia kitendo hicho.
Kutokana na kuwapo kwa hali hiyo, kamanda amewahimiza wa zazi mkoani Katavi kufuatilia vitendo anmbavyo wanaweza kuwa wamefanyiwa watoto wao na pia wazazi waache tabia ya kuamini imani potofu za kishirikina.