Katavi: Serikali waombwa kuingilia kati mgogoro wa ardhi, wadai wawekezaji wamepewa kinyume na utaratibu wa sheria

Katavi: Serikali waombwa kuingilia kati mgogoro wa ardhi, wadai wawekezaji wamepewa kinyume na utaratibu wa sheria

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
BAADH ya wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameiomba Serikali ya Mkoa huo kuingilia kati mgogoro wa ardhi wa zaidi ya hekali 40 zilizopo katika Kitongoji cha Jelemanga "A" na "D"kijini cha Milala.

Mgogoro huo uliodumu muda mrefu unatokana na baadhi ya wananchi kudai kuchukuliwa maeneo yao na Serikali ya Kijiji cha Milala na kugawiwa kwa wawekezaji mbalimbali kinyume na utaratibu wa sheria.

Miongoni mwa walalamikaj, John Alex Wangala akizungumza jana (Machi 13, 2022) akiwa kwenye eneo la mgogoro wa ardhi kijini hapo alisema anashangaa kuona eneo lao likigawiwa kwa watu na kufanyika ujenzi wa nyumba za makazi pamoja huduma za kijamii kama vile kanisa, shule ya mtu binafsi huku wakiwa hawajui taratibu zipi zimetumika kupewa maeneo hayo.

Wangala alifafanua kuwa baada ya kufuatilia kwenye uongozi wa Serikali ya Kijini cha Milala, Wenye mamlaka ya kijini walishidwa kutoa ufafanuzi huku wakidai kuwa maeneo hayo ni ya wazi na kuwa ni mali ya kijiji.

Wakati hayo yakiendelea, Wangala kwa kushinikiana na wananchi wengine wanaodai kuwa na uhalali wa umiliki wa maeneo hayo licha ya kuonesha nyaraka mbalimbali za kimaadishi zinazoonesha uhalali wa umiliki bado serikali ya kijini imeshindwa kutambua uhalali huo.

Lwenche Erenest aliweka wazi kuwa baada ya kuona hakuna msaada wanaopewa na Serikali ya kiji waliamua kwenda baraza la ardhi la Kata ya Misukumilo Manispaa ya Mpanda pamoja na mahakamani ambapo vyombo hivyo vya utoaji wa haki viliamuru eneo hilo kusitishwa uendelezaji wa shughuri zozote (Stop order) hadi pale ufumbuzi utakapo patikana.

"Hatuwezi kukubali kupoteza haki yetu kwa njama zozote zinazofanywa na Serikali ya kijji na wawekezaji dhidi yetu, Tuna uhalali wa umiliki wa ardhi hii kwa sababu nyaraka tunazo tena ambazo zingine zimetiwa saini na viongozi wa serikali ya Kijiji cha Milala 28, Novemba, 2010 ambapo mihutasari inayoonyesha uhalali wetu wa umiliki.. hatukubali viongozi watugeuke," alisema Erenest.

Anthony Mzoka alisema kwa kukili kuwa alinunua moja ya sehemu ya ardhi ya mgogoro ambapo aliuziwa na Serikali ya kiji (kiasi cha fedha hakuweka wazi) lakini baada ya kuona linamgogoro aliweza kuondoka huku akishangaa kwanini serikali ya kiji inaendelea kuuza maeneo hayo.

Mzoka aliomba Serikali ya kiji hicho kuingilia kati mzozo huo wa ardhi, kwani kama viongozi waliowapa dhamana ya kuwaongoza wanapaswa kutenda haki kwa wananchi wote huku akiiomba serikali ya Mkoa kuutatua kero hiyo isije kuhatarisha usalama wa watu.

Mwenyekiti wa Kiji cha Milala, Veronica Lemi alikiri kuwepo kwa mgogoro wa ardhi ambapo kama serikali hatua ilizozichukuwa ni pomoja na kusitisha zoezi la upimaji ambao uliwahi kuendeshwa ili kuacha ufumbuz upatikane.

Lemi akijibu madai ya Serikali ya kiji kuhodhii maeneo hayo bila utaratibu maalamu alisema kuwa historia inasema kuwa baadhi ya Babu zao wamiliki wa maeneo hayo na waliondoka kijini hapo mnamo mwaka 1960 ambapo mwaka 1970 kulifanyika operesheni ya upangaji wa viji lfanyika na eneo hilo la ardhi liliangukia kuwa miliki ya serikali ya kijji.

Aidha, mwenyekiti huyo alisema serikali ya kijiji kwa sasa ina utayari wa kusikiliza shauri la madai ya baadhi ya wananchi hao ingawa hakuna hati yoyote iliyowasilisha ofisini kwake ya kuzuio la uendelezaji wa shughuri za kibinadamu.

Diwani wa Kata ya Misikumilo Mansioaa ya Mpanda, Matondo Kanyepo alieleza kuwa anafahamu mgororo huo na wako katika hatua za kuutatua.

Kanyepo ameomba pande zote mbili kuvumilia wakati suluhisho la mgogoro huo ukiendelea kutafutiwa mwarobaini kila mmoja aweze kupata haki yake.

Source: Majira
 
Back
Top Bottom