KATAVI: Ujenzi wa meli nne za mizigo bandari ya Karema, umeanza

KATAVI: Ujenzi wa meli nne za mizigo bandari ya Karema, umeanza

President of China

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
34,781
Reaction score
94,550

View: https://youtu.be/7aPJ1GP9HI4?si=3qPt-dgtRClDyksg


Wabunge wanaotoka ukanda wa ziwa Tanganyika ikiwemo Katavi,Kigoma na Rukwa wakiongozwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile wamefanya ziara Mkoa wa Katavi katika Wilaya ya Tanganyika eneo la Bandari ya Karema, ambapo wametembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa Meli nne (4) za Mizigo zinazojengwa na Gold Voyage Logistics LTD Mwekezaji kutoka Nchini China.

Akiongea Mara baada ya ukaguzi huo Kihenzile amesema ujenzi wa Meli hizo unatarajiwa kukamilika ndani ya Miaka miwili na zitafanya shughuli katika Ziwa Tanganyika na kuhudumia Nchi zilizopo ukanda wa Ziwa hilo,"Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia imefanya kazi kubwa hatuna budi kuipongeza" sasa Ziwa Tanganyika itakuwa kimbilio la wengi kuja kuwekeza.

Wakati akitoa taarifa ya Mradi wa Bandari ya Karema Mkurugenzi wa Mipango mamlaka ya Bandari Tanzania Dr. Boniface Nobeji amesema wameingia mkataba wa Ujenzi wa Meli nne zenye uwezo wa kubeba Tani elfu mbili na Kampuni ya Gold Voyage Logistics LTD ya Nchini China ndani ya Miaka miwili, na Mkataba huo ni wa Upangishaji wa ujenga wa Meli hizo na TPA itapata kiasi Cha shilingi Dola mil.1 na 58 elfu kwa kulipia eneo hilo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa mwenyekiti Kamati ya bunge ya kudumu ya Uwekezaji Nickolaus Ngassa "kwa niaba ya Kamati wameridhishwa, tumeona tija ya Uwekezaji na tayari Bandari imeanza kufunguka, na ukishakuwa na wawekezaji maana yake tayari kile ambacho ulikipanga kifanyike na kitoe tija kimeanza kuonekana"-amesema.

Nae Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Katavi Martha Maliki ameishukuru Serikali na kuipongeza, kwani katika ujenzi wa Meli hizo tayari vijana wa Karema wamepata fursa ya kufanya kazi kwa Mwekezaji huyo na kuchochea Maendeleo katika Mkoa wa Katavi.
 
Back
Top Bottom