JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amezungumzia kuhusu matukio ya ukatili yanayotokea katika Mkoa huo, watoto wakiwa sehemu kubwa ya waathirika.
Amesema matukio 887 sawa na 65.17% ya matukio 1,361 yaliyoripotiwa kuanzia Januari hadi Machi 2022 yalihusu watoto.
Takwimu hizo zimeonesha kuna wastani wa watoto 9 wanafanyiwa ukatili na kunyanyaswa kila siku mkoani humo.
"Niombe familia kutenga muda wa kukaa pamoja, kujadili mambo ya kifamilia, kufanya uamuzi na mipango, hii inajenga upendo na mshikamano ikiwemo kufahamu maendeleo ya watoto nyumbani hadi shuleni na kuwapeleka sehemu za ibada, ili kujenga jamii imara," – anasema Mwanamvua na kuongeza:
"Nitoe rai kwa kila mwanafamilia kutimiza wajibu wake katika suala la malezi ili kuondokana na wimbi la familia zinazotelekezwa na watoto wa mtaani, familia ikipata mahitaji muhimu chakula, malazi, mavazi, ulinzi na upendo, ukatili hayawezi kutokea."