Katazo la kuandamana haliwahusu Simba ba Yanga ila CHADEMA pekee?

Katazo la kuandamana haliwahusu Simba ba Yanga ila CHADEMA pekee?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,982
Reaction score
51,157
Wakati mwingine huwa siwaelewi CCM wanaposema maandamano ni jambo baya. Au hawajui maandamano ni kitu gani!

Kuandamana ni mfuatano wa watu mmoja akimfuata mwingine. Sasa ubaya wa CHADEMA kuandamana unatokana na nini?

Kwa siku mbili mfululizo mashabiki wa Simba na Yanga wamekuwa wakifanya maandamano katikati ya Jiji la Dar es salaam bila ya kubughudhiwa badala yake wanasindikizwa na polisi.

Kwani CHADEMA wanazuiwa kuandamana wakati Simba na Yanga wanaruhusiwa. Jee tatizo ni maandamano ama tatizo ni nani anaandamana?
 
Ibara ya 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Ibara hiyo inasema:

"Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani..."

Hii ndiyo ibara inayotambuliwa kama msingi wa kikatiba wa uhuru wa kukusanyika na kuandamana kwa amani nchini Tanzania.
 
Mfano sasa hivi Uzi huu unapoenda hewani...Maelefu ya Mashabiki wa Simba na Club kwa ujumla wapo katika maandamano makubwa kutokea airport kuelekea CBD.

Hali hii ya maandamano imepelekea hali ya usafiri kuwa ya changamoto sana hasa kwa watu wanaolekea airport/gmboto maana wanakutana na msongamano wa maelfu ya waandamanaji wakielelea City center.

Inashangaza sana ile kauli ya "tishio la usalama" hai-apply kwa kina choendelea sasa hivi au hii ni kwa ajili ya vyama vinavyofanya mikutano kuikosoa serikali kwa madudu yanayoendelea nchini.

Sisiem sasa hivi wamesahazoea siasa za kudeka na kukosa uvumilivu.

Kila chochoro wamejaza polisi juani na mabunduki ya vitani kudeal na watakaoandamana kukosoa mabovu yanayoendelea ila kudhibiti maandamano ya Simba na Yanga aaagh...!
 
Wakati mwingine huwa siwaelewi CCM wanaposema maandamano ni jambo baya. Au hawajui maandamano ni kitu gani!

Kuandamana ni mfuatano wa watu mmoja akimfuata mwingine. Sasa ubaya wa CHADEMA kuandamana unatokana na nini?

Kwa siku mbili mfululizo mashabiki wa Simba na Yanga wamekuwa wakifanya maandamano katikati ya Jiji la Dar es salaam bila ya kubughudhiwa badala yake wanasindikizwa na polisi.

Kwani CHADEMA wanazuiwa kuandamana wakati Simba na Yanga wanaruhusiwa. Jee tatizo ni maandamano ama tatizo ni nani anaandamana?
Yaani bwana ukajichanganya unakuta Umekosea huku na kule umepatia🤣
 
Back
Top Bottom