Katazo la ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu sehemu za kazi

Katazo la ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu sehemu za kazi

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
234
Reaction score
376
Kumekuwa na kasumba mbaya ya kuwabagua watu wenye ulemavu kazini. Ubaguzi unaweza kufanywa na waajiri dhidi ya watu wenye ulemavu au kufanywa na waajiriwa wengine dhidi ya watu wenye ulemavu.

Ubaguzi kwa kigezo cha ulemavu au tofauti zozote katika sehemu ya kazi sio jambo linalotakiwa kutendeka.

Mwajiri hapaswi kumbagua mtu mwenye ulemavu tofauti na wafanyakazi wengine ambao hawana ulemavu.

Tangu mwanzo wa kutoa tangazo la ajira hadi pale watu wanapokuwa tayari katika ajira, ubaguzi wa aina yoyote hauruhusiwi. Hivyo, tangazo la ajira litolewe kwa misingi ya kutaka watu wote wenye sifa kupeleka maombi ya kazi. Kwa mfano haitakiwi tangazo liseme "Watu wenye ulemavu hawaruhusiwi kuomba kazi hii."

Mwajiri au taasisi yoyote iwe ya umma au binafsi wanapotangaza nafasi za kazi wanatakiwa kuhamasisha watu wenye ulemavu kuomba nafasi hiyo.

Baada ya kuajiriwa watu wote wanatakiwa kufahamu mashariti ya kazi na majukumu ya kazi kama inavyohitajika.

Malipo ya kazi hiyo ni lazima yawe wazi ili mwajiliwa atambue atapokea kiasi gani cha mshahara. Posho au marupurupu, likizo na haki nyingine muhimu kwa wafanyakazi ni lazima zitolewe kwa usawa pasipo kuwabagua watu wenye ulemavu.

Haki ya mafunzo, kujiendeleza, uamisho, kupandishwa cheo au kuacha kazi kwa hiari ni haki ya kila mfanyakazi. Pia, Mwajiri anatakiwa kumpatia vifaa wezeshi mtu mwenye ulemavu ili kusaidia katika utendaji wa kazi zake.

Ni kosa kwa Mwajiri yoyote kumbagua mtu mwenye ulemavu katika kazi, kwani kufanya hivyo ni kosa na atatakiwa kuwajibika kwa kulipa faini ya shilingi milioni mbili au kutumikia kifungo kwa miaka miwili au vyote kwa pamoja.

(rejea kusoma kifungu cha 33 cha sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010)

Imeandaliwa na:
Mr. George Francis
0713736006

Join us
Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓

Facebook: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓No. I
 
Mbona sijawahi kuona tangazo linalokataza watu wenye ulemavu kuomba kazi?
 
Back
Top Bottom