DidYouKnow
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 1,229
- 1,950
Uuguzi ni mojawapo ya kazi inayohitaji huruma na uwezo mkubwa wa akili. Kwa bahati mbaya sana, uuguzi Tanzania imekuwa ni sehemu ambayo wanaenda kusoma wahitimu wa masomo ya sekondari wenye ufaulu duni.
Tabia hii imewafanya wauguzi wawe ni watandika vitanda, wageuza wagonjwa, wasafisha wagonjwa na wafanya usafi kwenye maeneo ya kazi.
Wauguzi wengi huwa hawana uelewa wa kutosha wa magonjwa yanayowasibu wateja wao, na hivyo wao hufuata tu maelekezo toka kwa madaktari ambayo hawawezi ku-question hata siku moja. Hii ni hatari sana.
Bahati mbaya sana hawa wauguzi huenda kufanya kazi na madaktari, ambao nako sasa kumeanza kuharibika kwa kuwa na vyuo utitiri visivyo na sifa ambavyo huchukua kila mtu mwenye ndoto ya kuwa daktari kwenda kusomea udaktari hata kama ana ufaulu duni. Wengine wakishindwa kusomea Tanzania kutokana na ufaulu hafifu wanakimbilia China, Uturuki na nchi nyinginezo za Asia ambako kuna vyuo vidogo katika mataifa hayo, vinafanya biashara ya kutengeneza madaktari wasio na sifa.
Kina kitu kinapaswa kibadirike.