Katekista afanya viroja kanisani

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,970
Reaction score
35,168
Wale watakaonielewa kwa hii salamu basi waitikie.

Tumsifu Yesu Kristu.

Sijui nianze kwa kujiuliza swali, hivi siku hizi viongozi wa dini wamechoka kuenzi na kuzingatia maadili ya dini (zilizokuja nchini kutokea nchi za watu wa rangi nyeupe).

Ilikuwa ni maajabu makubwa sana jana kwa waumini walioshiriki ibada ya pili ambayo inaanza saa tatu asubuhi, Parokia ya Nyakato, Parokia Teule Buswelu.

Wakati wa kukomunika huwa wanakwaya wanaimba nyimbo ambazo zinaendana na tendo hilo wakiwa wanazingatia liturujia (katoliki watanielewa).

Waumini tulishikwa na mshangao pale Katekista Galashi alipoanza kuongoza kwaya ya mtakatifu Thomas (yeye huwa anaimbia kwaya ya mtakatifu Anna), wakati huo watu wanakomunika, akazidisha manjonjo ya ajabu ambayo hayako kwenye utaratibu wa ibada za kanisa katoliki! Manjonjo yalizidi hadi akafikia kuangalia altareni, akaanza kusujudu (kama waumini wa dini Fulani hivi wanavyosujudu kwa kugusa paji la uso ardhini wakiwa wanafanya sala zao).

Katekista Galashi alifanya vioja vingi sana, mwishowe nikasikia waumini wananong'ona chini kwa chini wakisema "HUYU ATAKUWA AMERUDIA ILE TABIA YAKE YA ULEVI WA KUPINDUKIA"

Namshukuru Padre kabla ya kuhitimisha misa alisema maneno haya "NINGEKUWA MIMI NDIE PAROKO, LEO HII KATEKISTA WENU WA BUSWELU ANGEKUWA HANA KAZI, LAKINI HATA HIVYO KATEKISTA JITAFAKARI..."

NAHUJA mie nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko.
 
Asamehewe tu, hakuna namna
Sijajua maana padre alichukia sana, kama wewe ni katoliki utapata picha halisi alivyotoa show ya ajabu, mpaka ule wakati wa kurudisha ekaristi "tabelinakuru" (mmmh! kilatini hiki), waumini wanapiga magoti kwa heshima, yeye hapo ndio akawa sasa kama ameaambiwa azishe "show" hahahaha ama kweli pombe sio chai.
 
Kwani rc si ni kawaida kwenda Ibadani na kulewa

Naonaga vioja kwenye mikesha ya Christmas na pasaka,,wanakwaya waumini wako njwiii,,,sio wote lakini
Ni kweli Roman Katoliki tunaruhusiwa kunywa pombe lakini mmmmh! sio kama za katekista jana! hahahahha. Ila huwa tunagonga kusema kweli
 
Hahaaa huyu sasa kazidi..Kwa akili ya kawaida I hope huko alipo anajutia alichofanya..Ingekua watoto wa mamdogo ingefaa achunjwe au apondwe mawe Mimi mwenyewe nilikoseaga kuitikia pale wanapisena Mwili wa yesu instead of Amin nikasema Tunauabudu..Nilikula kibao na sikupata kukomunika.
Paroko maduhu Mungu anakuona
 
Unatuanikia mambo ya kanisani kwenu ili tufanyeje sasa
 
Ni kweli Roman Katoliki tunaruhusiwa kunywa pombe lakini mmmmh! sio kama za katekista jana! hahahahha. Ila huwa tunagonga kusema kweli
Sema kila kitu kwa kiasi..pombe kwa kiasi, chakula kwa kiasi, maji soda juisi vyote kwa kiasi
 
hahahahahaaahah, Ilikuwa siku ya kwanza unapata komunio ndio ulikosea ukasema tunauabudu au ni baada ya kupata hiyo sakramenti ya komunio? hahahaah sipati picha wale walinzi wanaokaa pembeni ya padre walivyokutoa balu hahahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…