Wale watakaonielewa kwa hii salamu basi waitikie.
Tumsifu Yesu Kristu.
Sijui nianze kwa kujiuliza swali, hivi siku hizi viongozi wa dini wamechoka kuenzi na kuzingatia maadili ya dini (zilizokuja nchini kutokea nchi za watu wa rangi nyeupe).
Ilikuwa ni maajabu makubwa sana jana kwa waumini walioshiriki ibada ya pili ambayo inaanza saa tatu asubuhi, Parokia ya Nyakato, Parokia Teule Buswelu.
Wakati wa kukomunika huwa wanakwaya wanaimba nyimbo ambazo zinaendana na tendo hilo wakiwa wanazingatia liturujia (katoliki watanielewa).
Waumini tulishikwa na mshangao pale Katekista Galashi alipoanza kuongoza kwaya ya mtakatifu Thomas (yeye huwa anaimbia kwaya ya mtakatifu Anna), wakati huo watu wanakomunika, akazidisha manjonjo ya ajabu ambayo hayako kwenye utaratibu wa ibada za kanisa katoliki! Manjonjo yalizidi hadi akafikia kuangalia altareni, akaanza kusujudu (kama waumini wa dini Fulani hivi wanavyosujudu kwa kugusa paji la uso ardhini wakiwa wanafanya sala zao).
Katekista Galashi alifanya vioja vingi sana, mwishowe nikasikia waumini wananong'ona chini kwa chini wakisema "HUYU ATAKUWA AMERUDIA ILE TABIA YAKE YA ULEVI WA KUPINDUKIA"
Namshukuru Padre kabla ya kuhitimisha misa alisema maneno haya "NINGEKUWA MIMI NDIE PAROKO, LEO HII KATEKISTA WENU WA BUSWELU ANGEKUWA HANA KAZI, LAKINI HATA HIVYO KATEKISTA JITAFAKARI..."
NAHUJA mie nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko.