Katekista afanya viroja kanisani

Katekista afanya viroja kanisani

Milele Amina mtani..

Huyo katekista alipiga balimi nini??
mmh! sijui alikunywa kinywaji gani, ila wanaomjua wanasema alikuwa cha pombe akaacha, kwa hiyo siku ndio wakawa wanajiuliza na kushangaa kuwa kumbe karudia tena tabia yake ya ulevi!!!
 
kuna tofauti gani kati ya paroko na padri
Nikujibu kwa dhana ya ualimu

1. Mnaweza mkawa waalimu mna elimu sawa lakini Mmoja wenu akachaguliwa kuwa mwalimu mkuu

2. Kila paroko ni padre lakini sii kila padre ni paroko

3. Paroko ni padre aliyechaguliwa miongoni mwa mapadre kuwa mkuu wa parokia

4. Hivyo paroko ni sawa sawa na mwalimu mkuu ambaye huchaguliwa kuongoza shule na anawezekana akabadilishwa muda wowote na kuwa mwalimu wa kawaida
 
sawa sawa
 
Ndio maana mimi niliukimbia kabisa Ukatoliki... Sitaki kabisa hata kuusikia.
Ptuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Wala hujawahi kuwa katoliki, zaidi uko humu JF na ID yako kwa ajili ya kuponda ukatoliki
 
  • Thanks
Reactions: Ntu
Wale watakaonielewa kwa hii salamu basi waitikie.

Tumsifu Yesu Kristu.

Sijui nianze kwa kujiuliza swali, hivi siku hizi viongozi wa dini wamechoka kuenzi na kuzingatia maadili ya dini (zilizokuja nchini kutokea nchi za watu wa rangi nyeupe).

Ilikuwa ni maajabu makubwa sana jana kwa waumini walioshiriki ibada ya pili ambayo inaanza saa tatu asubuhi, Parokia ya Nyakato, Parokia Teule Buswelu.

Wakati wa kukomunika huwa wanakwaya wanaimba nyimbo ambazo zinaendana na tendo hilo wakiwa wanazingatia liturujia (katoliki watanielewa).

Waumini tulishikwa na mshangao pale Katekista Galashi alipoanza kuongoza kwaya ya mtakatifu Thomas (yeye huwa anaimbia kwaya ya mtakatifu Anna), wakati huo watu wanakomunika, akazidisha manjonjo ya ajabu ambayo hayako kwenye utaratibu wa ibada za kanisa katoliki! Manjonjo yalizidi hadi akafikia kuangalia altareni, akaanza kusujudu (kama waumini wa dini Fulani hivi wanavyosujudu kwa kugusa paji la uso ardhini wakiwa wanafanya sala zao).

Katekista Galashi alifanya vioja vingi sana, mwishowe nikasikia waumini wananong'ona chini kwa chini wakisema "HUYU ATAKUWA AMERUDIA ILE TABIA YAKE YA ULEVI WA KUPINDUKIA"

Namshukuru Padre kabla ya kuhitimisha misa alisema maneno haya "NINGEKUWA MIMI NDIE PAROKO, LEO HII KATEKISTA WENU WA BUSWELU ANGEKUWA HANA KAZI, LAKINI HATA HIVYO KATEKISTA JITAFAKARI..."

NAHUJA mie nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko.
Naomba huyo katekisti aachwe.,,,! Hiyo kazi ni ngumu mno....!
 
mmh! sijui alikunywa kinywaji gani, ila wanaomjua wanasema alikuwa cha pombe akaacha, kwa hiyo siku ndio wakawa wanajiuliza na kushangaa kuwa kumbe karudia tena tabia yake ya ulevi!!!
Dooh salaaale
 
Back
Top Bottom