Kati Bakari Mwamnyeto wa Yanga SC na Ibrahim Ame wa Simba SC, nani kafanikiwa zaidi kimpira?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Bakari Mwamnyeto Kasajiliwa kwa Bei ya juu na Yanga SC na Gari bovu ( japo aliambiwa ni jipya) ila anaishia tu Kucheza VPL, Mechi za Kirafiki za Chamazi na ile Michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar na kama akicheza Michuano ya Kimataifa basi ni ile tu inayohusisha Timu ya Taifa (Taifa Stars) pekee ambako na kwenyewe huko inasemekana huwa anaonekana ni Uchochoro kwa Washambuliaji na Mchezaji anayeongoza kwa Kuchomesha huku akiwa ni Mzoefu wa Kupanda Mabasi pekee.

Ibrahim Ame Kasajiliwa kwa Bei ya Kati (Kawaida) Simba SC ila anacheza VPL, anacheza sasa CL ya Afrika, anapata Posho Kubwa za Simba SC, anapanda sana Ndege ndani na nje ya Tanzania mara kwa mara, Mshahara wake hauchelewi Kuingizwa katika Akaunti yake, hakopwi na Klabu, katika Mgao wa Ushindi wa Jana dhidi ya FC Platinum wa Tsh 250 Million yupo na hata katika Pesa ambayo Simba SC inaenda Kupata kwa Kuingia Makundi Tsh 1.3 Billion pia ana Mgao wake.

Mimi siyo Mshabiki sana wa Mpira wa Tanzania na si Mshabiki wa Simba au Yanga au Azam, ila nitashukuru mkinijibu nani hapa amefanikiwa mno.
 
Ndani ya uwanja Bakari amefanikiwa kwakuwa ana uhakika wa namba na kucheza mara kwa mara.

Nje ya uwanja Ame amefanikiwa kulamba pesa za Mo kilaini hata kama hana uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza.

Yote kwa yote, mpira wa bongo magumashi tu
Je, unadhani Kimoyomoyo nani anamuonea Wivu wa Kimaendeleo Mwenzake na pengine angetamani ahamie Timu ya Mwenzake ili afaidike mno?
 
Hili li genta na ma I'd yako kila siku utakuwa jobless wewe pimbi
 
Bakari yupo CHAN na anauhakika wa namba Yanga & Taifa Stars

Ame anaungana na shabiki anaelipwa pesa ndefu kuliko mashabiki wote bongo (Morrison) kwenda Mapinduzi Cup akiwa na wida yake mfukoni
 
Ndani ya uwanja Bakari amefanikiwa kwakuwa ana uhakika wa namba na kucheza mara kwa mara.

Nje ya uwanja Ame amefanikiwa kulamba pesa za Mo kilaini hata kama hana uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza.

Yote kwa yote, mpira wa bongo magumashi tu
Suala la namba kwa Simba ni timu ngumu sana, hivyo usitegemee wachezaji watoke sehemu nyingine wapate namba kirahisi.

Nitajie mchezaji wa Yanga ambao wanaweza kupata namba moja kwa moja Simba, na kama wapo basi hawazidi watatu na tena sio kumaliza dkk 90 zote.
 
Hela za MO hizo Simba haipati kitu kwani kila kitu anagharamia yeye iwe posho,kambi au mishahara na huduma nyinginezo zote.
 
Ushindi kwa Platinum ndiyo unakupa jeuri yote hiyo.Tulia kwa kuwa umeenda kwenye makundi na Ligi bado inaendelea utapata majibu msimu huu Timu gani Ni bora .Mpaka sasa Ni Yanga kwani haijafungwa hata mechi moja na malengo yao msimu huu kuchukua kombe bila kupoteza mechi pamoja na yote Tusubiri muda utasema nani Ni nani msimu huu
 
Ko Yanga kutokufungwa ndo timu iliyofanikiwa hadi hapa?
Kwenye Luc akukosea kuwaita manyani. Simba akishinda vipolo vyake ana kua sawa na timu ambayo haijafungwa, sasa amefanikiwa nini? Ko simba ambayo imeingia group stage haijafanikiwa?
 
Taja wachezaji watatu pale Yanga ambao wanaweza kuanza kikosi cha kwanza Pale Simba SC? Na useme watacheza nafasi za wachezaji gani (Wachezaji gani watakaa bench ili hao wa Yanga wapate nafasi).
 
Wewe umeshindwa kuficha mbumbumbu wako!
 
Huyo Bakari mwenyewe ni straight kwenye first eleven ya Simba ila Ame hawezi kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga
 
Taja wachezaji watatu pale Yanga ambao wanaweza kuanza kikosi cha kwanza Pale Simba SC? Na useme watacheza nafasi za wachezaji gani (Wachezaji gani watakaa bench ili hao wa Yanga wapate nafasi).
Lamine vs Babu Onyango
Mwamnyeto vs mzee Wawa
Tunombe vs cha pombe
umetaka tukutajiie 03, ukitaka zaidi useme!
 
Ame amefanikiwa na atafanikiwa sana ukilinganisha na Mwamnyeto.

Japo hana uhakika wa kuanza katika kikosi cha Simba lakini anatumika katika Transformation ya Kikosi, Misimu miwili ijayo atakua mmoja wa wachezaj muhimu sana katika kikosi cha Simba.

Mwamnyeto ana uhakika wa Kuanza lakini Changamoto inakuja katika idadi ya Mashindano anayoshiriki, Pamoja na uhakika wa Maslahi katika Timu. Japo Yanga imeanza kuhakikisha maslahi kwa wachezaj wake lakin hatujui baada ya misimu miwili mbele itakuaje

Kwa ufupi Mwamnyeto yupo njiani kufuata mafanikio anayopata Ame kwa sasa😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…