Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mapigano mengine makali ya wenyewe kwa wenyewe yameibuka nchini Sudan.Safari hii ni kati ya general Abdel Fattah al-Burhan ambaye ndiye kiongozi wa nchi hiyo kwa sasa na mkuu wa jeshi. Mpinzani wake ni general Mohamed Hamdan Dagalo maarufu kama Hemeti na ambaye ndiye naibu katika utawala wa sasa unaitwa wa mpito kuelekea utawala wa kiraia.
Majeneralji wote hawa walikuwa ni sehemu ya uongozi wa kijeshi wakati wa utawala wa rais Omar albashir.Katika maandamano yaliyopelekea kuondolewa madarakani kwa albashiri general Burhani alijionesha kama mtu aliyewaonea huruma sana wananchi na hata kutembelea maeneo waliyokuwa wamejikushanya jijini Khartoum na kutaniana nao.
Kwa upande wake general Hemet alikwishashutumiwa na taasisi za kimataifa kama mshiriki mkuu wa mauwaj yanayotajwa kutokea Darfur na yeye alitajwa kama kiongozi wa Janjaweed. Katika uongozi wa baada ya kuondoka kwa albashir ambapo Hamdoh alikuwa kiongozi wa kiraia katika serikali hiyo,majenerali hao walishirikiana vizuri jambo ambalo halikudumu kwa muda mrefu kabla ya kutokea kutofahamiana tena kila mmoja akiwa na wafuasi wake na ambapo Hamdoh aliwekwa pembeni hapo mwaka juzi 2021.
General Hemet amekuwa na jeshi lake linaloitwa RSF ambalo ni mwendelezo wa vikosi tangu enzi za Albashir vilivyotumika kuzima uasi maeneo mbali mbali ya nchi hiyo ikiwemo Darfur.General Burhani pamoja na kuwa ni kiongozi wa kijeshi tangu enzi za Albashiri kwa sasa ndiye mkuu wa jeshi la ulinzi na mkuu wa nchi kuelekea utawala wa kiraia.
Kipengele kinachotajwa kupelekea kutoelewana kwa majenerali hao kwa sasa ni namna ya kuviingiza vikosi vya RSF katika jeshi rasmi la nchi na muda wake.Wakati Hemet akitaka iwe ni kitendo kinachotakiwa kiendelee kwa muda mrefu hata miaka 10 ijayo kutoa fursa ya kuaminiana na kupata ufanisi.Kwa upande wake general Burha ametaka iwe ni jambo la kufanyika kwa haraka.
Mbali na kutajwa kuwa alihusika na mauwaji ya Darfur,general Hemeti kwa sasa anatajwa kupokea misaada ya kijeshi kutoka Urusi baada ya kuwafungulia njia katika uendeshaji wa migodi ya dhahabu ya nchi hiyo wakati mwenzake Burhani akitajwa kuwa na ushirikiano mkubwa na vyama vya kisjiasa vya mrengo wa kiislamu vilivyowahi kutawala nchini humo.
Hapo juzi kulionekana harakati kubwa za vikosi vya RSF za kuhamisha silaha kuelekea maeneo tofauti ya nchi karibu na jiji la Khartoumj kitendo kilichotajwa na ujpande wa Burhan kuwa kumefanyika bila ushirikiano wa kijeshi na jeshi lake.Siku iliyofuata hapo juzi vita kamili vilianza huku Hemeti akitangaza kushikilia ikulu na viwanja vya ndege na upande wa Burhani kukanusha huku ukitumia ndege za kuvita kushambulia maeneo kadhaa ya jiji hilo.
general Mohamed Dagalo (Hemeti)
general Abdulfatah AlBurahan