Kati ya CCM na Samia nani tatizo au nyenzo kwa taifa letu

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,099
Reaction score
13,709
Rais Samia Suluhu Hassan, kama kiongozi yeyote, hata tofauti, si rahisi kumuelezea. Wapo wanaomsifia hadi inatia kinyaa.

Na wapo wanaomkosoa hadi inakuwa nongwa. Ukichuguza sintofahamu hii, unashindwa kuelewa kama tatizo ni yeye au CCM au vyote.

Kwa maoni yako, nini tatizo au ubora kwa taifa letu toka kwa kiongozi huyu na chama chake au hata sisi watanzania tunaogoma kukataa kuburuzwa na kunyanyaswa na badala yake baadhi yetu wakapwakia uchawa na kujikomba na kujipendekeza?
 
Kati ya spika na sauti yupi ana tatizo .
Jibu ili nimekupa mfano huko kwenu CCm mlivyo ndani na serikali mnayoshikilia.
 
Tatizo ni mfumo mbovu wa utawala kuanzia chamani hadi serikalini. Rais wa Tanzania ni mungu mtu. Hakuna wa kumgusa si chamani wala serikalini. Anauwezo wa kufanya analotaka bila kuzuiwa na mtu yeyote.
 
Rais Samia Suluhu Hassan, kama kiongozi yeyote, hata tofauti, si rahisi kumuelezea. Wapo wanaomsifia hadi inatia kinyaa.

Na wapo wanaomkosoa hadi inakuwa nongwa. Ukichuguza sintofahamu hii, unashindwa kuelewa kama tatizo ni yeye au CCM au vyote.

Kwa maoni yako, nini tatizo au ubora kwa taifa letu toka kwa kiongozi huyu na chama chake au hata sisi watanzania tunaogoma kukataa kuburuzwa na kunyanyaswa na badala yake baadhi yetu wakapwakia uchawa na kujikomba na kujipendekeza?
1. Tatizo la ccm wakurekebisha ni yeye lkn hana huo utashi, hivyo tatizo ni yeye.
2. Samia kama Samia naye ni tatizo, alivyoshughulikia suala la Gwajima amejivua nguo, ilikuwa itumike hekima ndogo tu kama alivyomzima kipindi cha chanjo ya corona.
 
Back
Top Bottom