Kati ya DED na DAS nani bosi wa mwingine?

DAS ana comand watu wachache directly lakini ni kama political post. DED anacomand wakuu wote wa idara japo yupo chini ya DAS kimantiki. Watumishi wote watamtii zaidi DED kuliko DAS
 
lakini kwa uhalisia DED ni kila kitu maana ndie mwenye mafungu ya maendeleo, mwenye miradi na pia watu. yaani kama katibu mkuu ndani ya wizara. DAS ni kazi ya ukaraani na umtumishi wa kisiasa. nimewahi kumkatalia mzee wa chama hii post ya DAS maana nilikuwa sina ajiara nikaenda kulia kwa mzee akaniniambia kuna nafasi ya DAS mkoa wa Nyanda za juu kusini baada ya kushaurina na wenye uzoefu wakaniambi kaka acha utumwa mwambie akupe ajira ktk shirika la umma au wizarani siyo huo utumwa. DAS hakipo katika muundo wa utumishi wa umma ni kama katibu tarafa tu.
 
Nimepata mkanganyiko kujua nani bosi wa mwenzake kati ya DAS na. DED naomba kuelemishwa mwenye kujua.

DED na DC wana ukubwa sawa ikiwa DED anaongoza team ya maendeleo ya serikali ya mitaa na DC ana own wananchi na maendeleo yao. Kwa nafasi ya uraisi wa wilaya DC anakuwa little above DED..

DAS ni msaidizi wa DC na mamlaka yake hayavuki kwa DED kwa namna yoyote ile unless anataka taarifa za maendeleo nk

Mara zote tumeona migongano kati ya DED na DC ila hutokuta mgongano kati ya DED na DAS

Kwa uelewa wangu mdogo i might be right... just sharing what i know
 
Nimepata mkanganyiko kujua nani bosi wa mwenzake kati ya DAS na. DED naomba kuelemishwa mwenye kujua.
Au wewe ndio tuliznguana pale halmashauri flani ukijifanya wewe ni boss wang nikakutoa knock out?
 
Mkuu nafikiri unamaanisha DAS. RAS ni Boss wa watumishi wote katika Mkoa including wa mashirika na Taasisi zote za Serikali na za umma.
Yap nilimaanisha DAS kama mtoa mada anavyolinganisha
 
Ndiyo DAS ni wa wilaya, mkurugenzi ni wa halmashauri.
 
Kiprotoco DAS mkubwa na ndio maana anauwezo WA kusimamia maDED zaidi ya mmoja kwa Wilaya zenye Halmashauri zaidi ya moja.
 
watumishi wa wilaya kwa maana ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya sio kwa upande wa DED.... Watumishi wa serikali kuu tu na sio wa serikali za mitaa
 
Kiprotoco DAS mkubwa na ndio maana anauwezo WA kusimamia maDED zaidi ya mmoja kwa Wilaya zenye Halmashauri zaidi ya moja.
DAS hana huo ukubwa.... DAS ni msaidizi wa majukumu ya DC.... Na ni mkuu wa Afisa Tawala (Wilaya), watumishi wa Ofisi ya mkuu wa wilaya na makatibu tarafa..... Hagusi file la mtumishi wowote wa Halmashauri wala hana mamlaka kwa DED

Mimi ni Afisa Utumishi Wilaya niko kwa DED
 

True and clear... hakuna ubishi... Ni kama Padri na shehe
 
Kimuundo hakuna DAS kuwa juu ya DED.... DC anaweza kujaribu ama kujifanya yuko juu ya DED ila DAS no
 
kiitifaki DED anaweza kuwa chini ya DC but not DAS... DC na DED wana almost same rank... Ila DC ni raisi wa Wilaya ndio inammeza DED
 
Swali la msingi hapa ni.. Je kuna haja ya kuwa na DED pamoja na DAS kwa wakati mmoja? au nyadhifa mojawapo ingefutwa tu.
DAS Ni afisa Tawala Wilaya, huyu yupo kwa DC. DED, Ni mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya.
Ni Mkuu wa alimashuri, wakuu wote wa idara huwajibika kwake.
 
Mfumo wa kuwa na DC, RC, RAS na DAS ulirithiwa kwa wakolonI na lengo la hawa viongozi lilikuwa kusimamia interest za kiongozi mkuu wa koloni enzi hizo au Governor kwenye majimbo husika. Hizi local government ziliundwa mahsusi kutoa nafasi kwa machief kuwasimamia watu wao chini ya usimamizi na miongozo ya DC na team yake.
 
Mkuu, Umenukuu Kifungu cha 22(2) cha Local Government Service Act No. 10 of 1982 ambacho kinampa mamlaka Mhe Rais kuteua wakurugenzi ambao wapo kwenye Category VI to VII na wakurugenzi hao waliokusudiwa hapa ni wa manispaa na majiji (Municipal Directors na City Directors).

Hebu cheki na Kifungu kidogo cha 3 hapo chini yaani 22(3) utaona kuwa Waziri wa TAMISEMI ndiye mamlaka ya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya (DEDs) .

Hata awamu zilizopita, wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya walikuwa wakiteuliwa na Waziri wa TAMISEMI isipokuwa wale wa majiji na manispaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…