Super Handsome
JF-Expert Member
- Jul 16, 2013
- 3,844
- 6,448
DC DED na DAS tofauti yao ni Laki kama na ishirini hivi same to RC, RAS, PS!DED na DAS wanapoteuliwa na kuanza kazi kwa pamoja nani anakuwa juu kimshahara kumzidi mwenzake.?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
DC DED na DAS tofauti yao ni Laki kama na ishirini hivi same to RC, RAS, PS!DED na DAS wanapoteuliwa na kuanza kazi kwa pamoja nani anakuwa juu kimshahara kumzidi mwenzake.?
PS ni nani?DC DED na DAS tofauti yao ni Laki kama na ishirini hivi same to RC, RAS, PS!
Kweli nimeamini kwamba ujinga ni Sawa na zigo la mavi, na uaipo lishusha kwa uzito wake basi utalituwa kwa harufu yake.......DED na DAS wanapoteuliwa na kuanza kazi kwa pamoja nani anakuwa juu kimshahara kumzidi mwenzake.?
Kijana, huku kuchamba kwingi kutakufanya ushike hajakubwa.... tehteehhhDED na DAS wanapoteuliwa na kuanza kazi kwa pamoja nani anakuwa juu kimshahara kumzidi mwenzake.?
Nisaidie link mkuu!!
Idadi ya madc ni 5 pia?
PS permanent secretary, mshahara wa RC ni 3.6PS ni nani?
Afu mbona nasikia mshahara wa RC na waziri hawatofautiani sana?
Hata mwaka haujaisha mmeingia kwenye mgogoro. Umetoka kuuliza nani ni boss kati ya DAS na DED... ghafla umehamia kwenye mshahara[emoji23] [emoji23] [emoji23]DED na DAS wanapoteuliwa na kuanza kazi kwa pamoja nani anakuwa juu kimshahara kumzidi mwenzake.?
RC anakula 6.8-7MPS permanent secretary, mshahara wa RC ni 3.6
Sijui kama upo sahihi sana, ninavyojua ni kwamba DAS ni human resource administrator ktk level ya wilaya, kwenye mashirika umma tunawaita HR. Juu yao kuna watendaji yaani Mkurugenzi. Wilayani kuna Mkurugenzi wa halmashauri yaani DED, kweli mashirika ya umma kuna Mkurugenzi mkuu.DAS anawajibika kwa RAS, hali kadhalika DED. Hivyo hakuna line ya uwajibikaji wa moja kwa moja wa DED kwa DAS. Hata hivyo kiitifaki DAS yupo juu zaidi ya DED.
Niongeze kwamba DAS anauwezo wa kumuita DED ofisini kwake na akamuagiza cha kufanya. Lakini DED hawezi kufanya hivyo kwa DAS.
Hakuna wilaya zenye halmashauri mbili, bali wilaya yenye majimbo mawili
Na zina ma ded wake?Wilaya ya Kahama INA halmashauri tatu za msalala, ushetu na kahama.
Wilaya ya Babati INA halmashauri mbili za Babati TC na DC.
Ndiyo, mbona zipo wilaya kibao tu zina halmashauri zaidi ya moja! DC mmoja, DAS mmoja, wakurugenzi wa Halmashauri wawili na pengine watatu.Na zina ma ded wake?
Asante mkuu, nimekueleawaNdiyo, mbona zipo wilaya kibao tu zina halmashauri zaidi ya moja! DC mmoja, DAS mmoja, wakurugenzi wa Halmashauri wawili na pengine watatu.
Mfano ni hiyo wilaya ya kahama ina wakurugenzi wa halmashauri watatu
DC, maana yeye ndiye raisi wa wilaya.DED = District Executive Director, DAS = District Administrative Secretary & DC = District Commissioner. Wote hao ni kuteuliwa na kutumbuliwa wakati wowote. Nani mkubwa hapo
Asante sana Mkuu. Pia DC ni political figure wakati DED ni Mtendaji na anamiliki rasilimali. DAS ni arm ya DC na uteuzi wake ni Waziri wa Utumishi hivyo huwezi kuwa juu ya DED mteule wa Rais. Kiukweli DAS wako redundant kidogo wala hawaonekani sana kwa kuwa wamegunikwa na DC na DED. Hivyo basi DAS huwezi kufuatwa na DED kiprotokali kabisa. DED anaweza kumfuata DC tu na pia siyo lazima. Tena bora miaka hii DC wanasikika. Huko nyuma DC walikuwa ni shida na wakati mwingine utawakuta wamekaa kwa DED kwa kuwa huko ndiko mapeni yapo. Na UTARATIBU wa kimuundo ni DED kwa RAS na DAS kwa DC.Wadungu naomba nami nichangie mada hii ambayo wengi wanaona kama uhusiano wa DED na DAS ki-protokali unachanganya. Mchango wangu utazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.
1. Mkuu wa Wilaya (DC)
Mkuu wa Wilaya anateuliwa na Raisi kwa mujibu wa kifungu cha 13 (2) cha sheria ya Tawala za Mikoa (The Regional Adminstration Act, 1997). Majukumu yake ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya. Kwa mantiki hiyo anakuwa muwakilishi wa Raisi katika kusimamia ulinzi, usalama na shughuli za maendeleo kwa ujumla. Akishateuliwa mkuu wa Wilaya anaapishwa na kusimamiwa kiutendaji na mkuu wa Mkoa (kifungu 13 kifungu kidogo cha 3).
2. Katibu Tawala wa Wilaya (DAS)
Kifungu cha 16 (2) cha sheria ya Tawala za Mikoa kinamtambua DAS kama principal adviser (yaani mshauri mkuu) wa DC. Kifungu hiki pia kinasema DAS anateuliwa kwamujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma. Bahati mbaya sina hiyo sheria hapa na nimetafuta mtandaoni sijaweza kuipakua. Ila natoa hoja yangu hapa kwa kuzingatia uteuzi wa Ma-DAS uliofanywa tarehe 5.8.2018 na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma. Katika tangazo lake kifungu cha 1.2 Waziri alisema, "Leo nimewaita kuzungumza nanyi kuhusu Uteuzi na Uhamisho wa baadhi ya Makatibu Tawala wa Wilaya. Kwa mamlaka niliyokasimiwa kwa mujibu wa Sheria nimefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya ili kujaza nafasi wazi kumi nane (18) zilizopo katika wilaya za Kinondoni, Mpwapwa, Dodoma, Iringa, Bukoba, Kigoma, Siha, Mtwara, Newala, Misungwi, Njombe, Kondoa, Manyoni, Kilindi, Chunya, Pangani, Bagamoyo na Handeni".
Hivyo, kwamujibu wa tangazo la Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma ambalo nimenukuu hapa, uteuzi wa DAS upo chini yake kisheria.
3. Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya (DED)
Kwa mujibu wa kifungu cha 22 (2) cha Sheria ya Utumishi wa Serikali za Mitaa ( The Local Government Service Act, 1982), DED anateuliwa na Raisi. Majukumu kiutendaji DED anakuwa Chief Executive wa Halmashauri na anaripoti kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS).
Hitimisho
Kwangu mimi sioni mkanganyiko wowote wa kisheria kati ya DED na DAS, maana DED anateuliwa na Raisi na DAS anateuliwa na Waziri wa Utumishi wa Umma. Sema DAS anaweza kuonekana katika mazingira flani kuwa boss wa DED pale ambapo anatekeleza kazi anazotumwa na DC. Pia, nimewahi kuona mahala DAS anaudhuria vikao vya Council Management (CMT) ambavyo DED ndio mwenyekiti. DC ni mkuu kiitifiki kwa DED ingawa wote wanateuliwa na Rais, utofauti wao unatokana na majukumu. DC anapolinda amani, usalama na maendeleo ni pamoja na kazi anazofanya DED na wakuu wengine wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kwenye ngazi ya Wilaya.
Huu ni uelewa wangu kwa kadri nilivyoelewa sheria husika, kama kuna mahala nimekosea niko tayari kukosoloewa maana mimi si mwanasheria kitaaluma. Asanteni
Mkuu wa Mkoa ni sawa na Waziri, na ana wafanyakazi wake ambao ni RAS, DAS, DC na Assistant RASs na watumishi wengine.Rc, RAS zipo chini ya wizara gani? Sio tamisemi? (Tawala za mikoa na serikali za mitaa?)
Niliona Jafo akiagiza Ma RC.
Pia mbona nilishaona RC akimsimamisha ded kwa uchunguzi?
Ikitokea umeteuliwa RAS, na uiatumbuliwa, je utaendelea kupokea mshahara? Au utapangiwa kazi nyingine? Usipopangiwa kazi nyingine utakuwa unakaa nyumbani tu?Mkuu wa Mkoa ni sawa na Waziri, na ana wafanyakazi wake ambao ni RAS, DAS, DC na Assistant RASs na watumishi wengine.
Kwa hiyo Waziri hawezi kumfukuza kazi au kum-critcize mkuu wa mkoa and viceversa.
Lakini anaweza kufanya hivyo kwa DED.
Unakuwa huna kazi wala mshahara.Ikitokea umeteuliwa RAS, na uiatumbuliwa, je utaendelea kupokea mshahara? Au utapangiwa kazi nyingine? Usipopangiwa kazi nyingine utakuwa unakaa nyumbani tu?
Je Mtu kama Mafuru aliekuwa Mkuu wa hazina, alivyotumbuliwa na huku hatujasikia akipata uteuzi mwingine anaebdelea kulipwa mshahara? Anashinda nyumbani tu?