Nestory Yamungu
Member
- May 20, 2017
- 85
- 75
Nahisi tunanukuu sheria mbili tofauti, The Local Government Service Act ya 1982 niliyotumia inasema hivi, nanukuu kifungu cha 22 kifungu kidogo cha kwanza na cha piliMkuu, Umenukuu Kifungu cha 22(2) cha Local Government Service Act No. 10 of 1982 ambacho kinampa mamlaka Mhe Rais kuteua wakurugenzi ambao wapo kwenye Category VI to VII na wakurugenzi hao waliokusudiwa hapa ni wa manispaa na majiji (Municipal Directors na City Directors).
Hebu cheki na Kifungu kidogo cha 3 hapo chini yaani 22(3) utaona kuwa Waziri wa TAMISEMI ndiye mamlaka ya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya (DEDs) .
Hata awamu zilizopita, wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya walikuwa wakiteuliwa na Waziri wa TAMISEMI isipokuwa wale wa majiji na manispaa.
Section 22 (1) "There shall be a District Executive Director for each district".
Section 22 (2) "The Director shall be appointed by the President, on the advice of the Commission, upon such terms and conditions as the President may specify in the instrument of appointment".
Kifungu cha 32 (2) The President shall, on the advice of the Commission, appoint in respect of each Town, Municipal or City Council, Director".
Kifungu cha 22(3) ulichoniambia nisome kinasema "The Director shall, subject to this Act and to the general or specific directions of the district council, be the chief executive officer of the council and shall be answerable to the council for the discharge and exercise of his functions and powers"
Labda kama umesom sheria iliyofanyiwa marekebisho ila kwahii ya mwaka 1982 wakurugenzi wa wilaya (DED) wanateuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 22(2), wakati wale wa mamlaka za miji wanateuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 32(2). Ebu angalia vizuri, ingawa nakiri kuwa kuna inawezekana sheria ikawa imefanyiwa marekebisho maana hii ninayonukuu ni ya siku nyingi.