Una haki ya kuchanganyikiwa mkuu,hata mimi huwa nachanyikiwa,lakini naona kama wako at par,ingawa wakati mwingine naona kwa vile DAS ndiye kiongozi wa watumishi wote Wilayani,basi DED yuko chini ya DAS.Inachanganya kwa kweli.
Mimi huwa nadhani kuna haja ya kufuta mfumo wa kuwa na Halimashauri, ili kuondoa huo mkanganyiko ambao kiukweli unaleta misuguano na mikanganyiko isiyo ya lazima na hivyo kukwamisha utendaji kwa ujumla.Hivi kwa nini tusiwe na DC na DAS tu na chini ya DAS kukawa na idara mbali mbali ambazo zitashuhulikia issues za Willaya?Huu mfumo wa kuwa na Halimashauri unaongeza tu bureaucracy,matumizi ya fedha yasiyo ya lazima,ugumu wa udhibibiti na hivyo kuongeza uwezekano wa upigaji.Kwa ujumla mfumo huu uko inefficient.
Binafsi sioni faida za msingi za Halimashauri,infact naona kama they are just a liability to the government.
Halimashauri zetu zimeshindwa kabisa ku-meet expectations za Watanzania.