Habari za muda huu wakuu,
Naomba mnisaidie kujibu swali tajwa hapo juu, ipi ni kozi nzuri kusoma Kati ya hizo kwenye nyanja ya kuajiriwa pamoja na kuajiriwa.
Japo lengo langu kubwa ni kujiajiri.
Karibuni kwa michango yenu
Shukran kwa ushauri mzuri mkuu, vipi kuhusu suala la mionzi nasikia Ina madhara ,au ni maneno ya watu tuKwa sasa kozi za radiology zina wataalamu wachache ukilinganisha na laboratory.
Kwa hiyo unaweza kupata ajira kwa urahisi kwa kozi za radiology kuliko laboratory.
Kwa upande wa kujiajiri kwa mtazamo wangu naona radiology ina fursa kubwa ukilinganisha na laboratory. Mfano radiology (sonographer) ukiwa ultrasound machine nk unaweza kutoa huduma hiyo hata nyumba kwa nyumba au kwenye vituo vya afya binafsi kwa makubaliano maalumu.
Kwa hiyo ukiwa mzuri katika ujuzi wa mambo ya radiology na mtaji unaweza ukajiajiri.
Mwisho, ni muhimu sana ukasomea kozi ambayo unaipenda kwa moyo wako.
Kila la kheri.
Vip kuhusu mionzi nasikia Ina madhara au,ni maneno ya watu tu.Radiology is the best at the moment. Usijiulize mara mbili mkuu
Sikuhizi vifaa vinekuwa vya kisasa zaidi masuala ya mionzi yashakuwa story za zamaniVip kuhusu mionzi nasikia Ina madhara au,ni maneno ya watu tu.
Asante kwa ushauri wako mkuuSikuhizi vifaa vinekuwa vya kisasa zaidi masuala ya mionzi yashakuwa story za zamani
Nakupa Usahuri nikiwa nipo Kwenye hii Career ya Afya kwanza kabisa sikiliza wapi mapenzi yako yalipo
Pili suala la Ajira kwa uharaka ni 50/50 zote hizo hadi unamaliza ajira zake si za uhakika 100% why Radiology kwasasa vyuo vya kati bi vingi sana vimeanza kutoa tofauti na miaka 5 nyuma walikuwa ni MuHAS na CuHAS tu pia naangalia na uhitaji wake kwakituo kimoja mfano RRH kuwa na sonogralhers 10 ni wengi sana!!
Kujiajiri Laboratory ni cheap zaidi ukilinganisha na Radiology!!
Ila ukiwa competent enough na mjanja utaanza kula Peaa ya Radiology mapema sana hasa kama Upo mjini!
Kama kwenu uwezo mzuri. Kasome DDR haraka ila chagua Vyuo vikubwa kama MuHAS, CUHAS na Benjamin Mkapa!!