Kati ya hizi Nyimbo za Diamond alizowaimbia Zari na Wema, zipi zilikuwa Kali, je ndo alipendwa zaidi

Kati ya hizi Nyimbo za Diamond alizowaimbia Zari na Wema, zipi zilikuwa Kali, je ndo alipendwa zaidi

"UKIMWONA" ni bonge moja la pini, hasa beti la pili msengerema anajua yule
Hakuna wimbo wake ambao utakuja fikia ukimwona Manecky ile beat aliitendea haki halafu kutoumalizia ukavujishwa ukiwa na hanging chorus it was a blessing in disguise maana ulipendeza sana.
Toka 2012 mpaka leo nausikiliza na huwa haushi uzuri
 
THE BEST OF DIAMOND PLATNUMZ
1. I MISS YOU ndo the best song kwangu, ikifuatiwa na
2. UKIMUONA

Ila kati ya nyimbo ambazo Mond alikaa akatulia kwenye kutunga ni
3. BINADAMU WABAYA...
Huyu jamaa ni konyo. Huu wimbo naweza sema ni "Living Ghost", na natamani huu wimbo autolee version mpya na ya kisasa kwa beat la p-funk

4. NALIA NA MENGI akiwa na chid benzino, hii ni hatari nyingine katika masikio ya wengi

Nimalizie na
5. MDOGOMDOGO

Kwenye kuvuka boda, (nikimaanisha kolabo na wasanii nje ya bongo) hizi ndo hits nazozikubali;
1. INAMA dance na meseji yake n moto wa kuotea mbali

2. AFRICAN BEAUTY; huu ulistahili tuzo ya grammy

3. WAKA WAKA; ngeli iliyocharazwa humo ikanfanya nsahau kabisa kama Mond anatokea tandale

4. HALELUJAH; Reggae moja matata sana na iliwafanya wajamaika kuipandisha chat mpaka karibia 10 bora kati ya 100

5. NANA/SOUND

Huyu kijana ni noma, kilichobaki sasa ndo hiki cha kushindanisha nyimbo zake, maana sioni wa kushindana naye kibongobongo
 
Huyu jamaa kuna habari zina sema ameanza kula poda.[emoji848][emoji848]

Ni nje ya mada .
 
Mimi naipenda Inama ya fally i pupa
Hiyo niache nadhani alimwimbia hamiasa mobetto.
I stand to be corrected.

Ilikuwa diss kwa hamisa, Ila Zari aamini kuwa hampendi na hamtaki hamisa, yani aliimba vile kumplease zari
 
Moyo wangu kwa Wema was lit, Kisha Ntampata wapi (cjui aliimbiwa nani), kisha number 1 og (cjui qliimbiwa nani), kisha Ukimuona kwa Wema was lit, kisha Mawazo kwa Jacline wolper was fire...

kiufupi jamaa ngoma zote za albam yake ya kwwnza na zile za kuchia kawaida zilikuwa noma sana kipindi hiko.
 
sahau nyimbo zooote za diamond ila sio
NTAMPATA WAPI
Ukimwona
I miss you
lala salama
the one
 
Back
Top Bottom