Kati ya Ivory Coast na Tanzania ipi imepiga hatua zaidi kimaendeleo?

Kati ya Ivory Coast na Tanzania ipi imepiga hatua zaidi kimaendeleo?

Ivory Coast Iko mbali ya Tzn siku nyingi sana kuanzia miundombinu Hadi maisha.

Tzn ni Kati ya Nchi 5 Zenye namba kuumbwa ya maskini Afrika Sasa hapo GDP inakusaidia nini?

Ivory Coast Iko mbela ya Tzn Kwa Kila idara,hata Jiji la Abidjan ni kubwa na Lina maendeleo kuliko Dar sio Kwa idadi ya watu Wala miundombinu au majengo marefu.

View: https://youtu.be/OepYPIjyDgQ?si=KFx5r4GOWw2nR-sF


hiyo picha uliyoweka ya kawaida sana, Kwa mtu mwenye taaluma ya picha hapo ameonesha sehemu kidogo sana ya mji kama 10% akawa anarudia rudia; Ina maana huko kwingine hakuko poa. Ukiamua kupiga picha Dar ya kuonesha sehemu kidogo hivyo itaonekana nzuri mara mbili ya hiyo picha....
 
Tanzania ni habari nyingine.
Japo kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja (per capital income) wametuzidi but
Gdp na ppp yetu ni kubwa kuliko wao.
Nchi za West Africa ni Nigeria tu ndio atatutetemesha
Mkuu acha Comedy bhasi..
Maana umenichekesha sana 😅😅😅
 
Ivory Coast Iko mbali ya Tzn siku nyingi sana kuanzia miundombinu Hadi maisha.

Tzn ni Kati ya Nchi 5 Zenye namba kuumbwa ya maskini Afrika Sasa hapo GDP inakusaidia nini?

Ivory Coast Iko mbela ya Tzn Kwa Kila idara,hata Jiji la Abidjan ni kubwa na Lina maendeleo kuliko Dar sio Kwa idadi ya watu Wala miundombinu au majengo marefu.

View: https://youtu.be/OepYPIjyDgQ?si=KFx5r4GOWw2nR-sF

Mkuu 👏👏👏👏👏👏
Naomba niseme Kwa leo umenifurahisha sana sikuamini kama Wewe ungeandika hivi
 
Mchawi mkuu anayekwamisha maendeleo nchini, ni ccm. Bila ya uwepo wake, huenda mpaka muda huu tungekuwa mbali sana.

Imagine tuna raslimali za kila aina! Ila mwisho wa siku mchwa hatari wanaoitwa ccm, wanazitafuna tu peke yao! huku mamilioni ya wananchi wakiendelea kuishi maisha ya kimasikini.
 
Ivory kosti
82329549-CEEF-46B3-934B-4E930E49D839.jpeg
 
Nimeona Wengi wanaubishi wa Kizalendo Anywei ni mzuri kwa sababu kusifia nchi yako ndio kitu Tunajifunza kila siku..

Ila tusifanye uzalendo ukatufumba macho kwenye sehemu pa kujifunza tukataka kuwa Walimu (Hapo ndo tunaharibu sana Watanzania)..

Tunajiaminisha tuna ukubwa ambao kiukweli hatuna..

Any wei naenda kwenye Point moja kwa Moja..

Kwa Mujibu wa Uchambuzi wa Sources Za Taarifa na Data mbalimbali Ivory coast na Tanzania Wanapishana Percent chache tu nitazielezea hapo chini

Ivory coast Ina 82% wakati Tanzania ina 74% kwenye ulinganisho huo..
Screenshot_20240114_104321_Chrome.jpg


Nitaanza kuzidiscuss Comparison hizo baadae ili tushee wote.. japo kwa kifupi ni hizi hapa chini.
Screenshot_20240114_104433_Chrome.jpg


Na hizo ndo Point walizostick nazo na nitazidiscuss zote moja moja..

pet96 Mparee2 ChoiceVariable Sultan MackJoe Khalifa saigilomagema
 
Kijiographia (Geographically)

  • Tanzania ina Eneo la 947 300 km² wakati Ivory coast in 322 463 km² tu..
  • Eneo la Tanzania limekuwa covered na misitu kwa 37.3% na wakati Ivory coast ni 32.7%..
  • Eneo linalotumika kwa ajili ya Kilimo ni 43.7% kwa Tanzania na 64.5% kwa Ivory coast
  • Eneo Lililo na ufukwe (Coustline) Yaani Karibu na bahari au beach kwa Tanzania ni 1424 Km wakati kwa Ivory coast ni 515 Km..
  • Eneo la Tanzania Nchi kavu Ukitoa bahari na Maziwa ni 885 800 Km² na Eneo la Ivory coast ni 318 003 Km²
  • Eneo lilitawaliwa na Maji kama maziwa,Bahari na mito kwa Tanzania ni 61500 km² na kwa ivory coast ni 4460 km²

Kidemographia (Demographically)

  • Tanzania ina watu wapatao Milioni 61 na Ivory coast in watu wapatao 26 Milioni
  • Population Density kwa Tanzania ni 59 People per km² (59 people/km²) Ila kwa Ivory coast ni 80 people/km²
  • Anual population growth rate kwa Tanzania ni 2.74% na kwa Ivory coast ni 2.3%
  • Life expectancy at birth kwa Tanzania ni miaka 63 na kwa Ivory coastni miaka 61
    • Life expectancy kwa Wanawake ni miaka 64.6 na kwa wanaume ni miaka 61 hiyo ni kwa Tanzania na Miaka 62.5 kwa wanawake na 58 kwa wanaume hiyo ni kwa Ivory coast..
  • Dealth Rate kwa Tanzania ni 7.5/1000 na kwa Ivory coast ni 8.4/1000


Sasa hivi ndo za kwanza za muhimu kabla hatujaingia kwenye Economy, Quality of Living na Infrastructure

Lakini kama ukiangalia kwa umakini utagundua kitu kwa watu wazee wa uchambuzi wa uchumi na analytical wa M&E

pet96 Mparee2 ChoiceVariable Sultan MackJoe Khalifa saigilomagema
 
Swali hapa why Ivory coast wawe better kuliko Mali na Burkina Faso??
Wakati wote wametawaliwa na ufaransa??
 
Economically (Kiuchumi)

  • GDP per capita ya Tanzania ni Dola za 3574 (3574$) Wakati kwa Ivory coast ni 4155$
(The GDP per capita inapatikana kwa kuchukua total GDP na kuigawanya kwa the number of people living in the country.)

Tukumbushane kuwa A higher GDP per capita indicates a superior standard of living..

So hii ndo point ya kwanza Wa Ivory coast walipotutwangia hapa wao wako wachache sana kulikp sisi....Maendeleo yanatakiwa Yaendane na Maisha halisia ya watu..


  • The GDP growth rate ya Tanzania kwa Sasa ni 6.7 wakati ya Ivory Coast ni 7 .8..
  • GINI index kwa Tanzania ni 40.5 wakati kwa ivory coast ni 37.2
    • (The Gini Index represents a statistical measure used to assess income inequality within a country.
    • It quantifies the distribution of income or wealth among the population, with a higher Gini Index indicating a greater level of inequality, while a lower index suggests a more equitable distribution. Source: The World Bank, 2024)
    • Kwahyo Tanzania kuna low Equatable Distribution ya wealth au Maisha Tanzania maskini anaendelea kukandamizwa na Tajiri anazidi kuwa tajri, Wakati Kwa ivory coast kidogo wamedevelop
  • Economic Freedom index kwa Tanzania ni 60 na kwa IVORY COAST ni 60.4 almost the same(Source: The Heritage Foundation 2024)
  • Kwenye upande wa Madeni Sasa Tanzania ana 37% Ya GDP yake ni Deni la Taifa na Kwa ivory coast ni 47% kwahyo hawa wajamaa wanakopa kuliko sisi.
  • Unemployment rate kwa Tanzania ni 10.3% na kwa ivory coast ni 9.4%
  • Education Expanditure kwa Tanzania wanatumia 3.5% Ya the whole GDP na kwa Ivory coast wanatumia 4.4% ya whole GDP
  • Health expenditure almost the same kwa sababu wote tunatumia 4% ya GDP
  • Labour force Tanznia ni 24.89 Milion wakati kwa ivory Coast ni 8.75 Milion (Hapa napo wametupiga bao kubwa sana kama wameweza kutuzidi vitu hivi au kukaribiana nao wakiwa na labour force ndogo namna hii)

  • kwenye GDP (Gross Domestic Product) kwa Tanzania Tuna 186.06$ bilion na Ivory Coast ina 106 .41 $Bilion (The Gross Domestic Product (GDP) reflects the value and productivity of an economy. It measures the market value of all the final goods and services produced annually. To reflect the differences in the cost of living and inflation rates, we show the GDP at purchasing power parity (PPP). Sources: Wikipedia, CIA World Factbook, 2024.)

  • CORRUPTION Perception Index (CPI) kwa Tanzania ni 38 na kwa ivory Coast ni 37
Viko vingi sana lakini kiukweli Jamaa wametuzidi kiasi kwenye vitu vingi ila nao tumewazidi..
ILA UCHUMI WA KWELI NA WA WA MAENDELEO NI GDP PER CAPITA na wao wametuzidi..


soma zaidi..

pet96 Mparee2 ChoiceVariable Sultan MackJoe Khalifa saigilomagema
 
Back
Top Bottom