Kati ya Julai 2023 hadi Aprili 2024 kulikuwa na Kesi 1,034 za Watu wasiotunza Watoto wao

Kati ya Julai 2023 hadi Aprili 2024 kulikuwa na Kesi 1,034 za Watu wasiotunza Watoto wao

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kuhusu huduma za Mahakama kwa watoto, Wizara imeendelea kuratibu huduma za Ustawi wa Jamii katika Mahakama za Watoto 133 nchini.

Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024, mashauri 4,462 yalipokelewa yakijumuisha mashauri 1,034 ya matunzo (maintenance), 952 ya uangalizi wa mtoto (custody), 882 ya kuona watoto (access), 680 watoto waliokinzana na sheria, 13 ya kuasili, 7 ya vinasaba (DNA order), 22 ya uthibitisho wa baba (parentage), na 872 ya huduma za afya ya akili, msaada wa kisaikolojia na kijamii (Mental Health and Psycho-social support - MHPS).

Jumla ya mashauri 3,984 kati ya yote yaliyopokelewa yalisikilizwa na kufungwa, na mashauri 478 yaliyobaki bado yanaendelea kusikilizwa.

Pia Soma:

 
Back
Top Bottom