Chukua SAMSUNG achana na hizo 4k ila za kidwanzi tu,
mimi niliacha Hisense 4k ya bei ndogo halafu nikachukua SAMSUNG FHD bei kubwa 200000 zaidi ila screen size ileile. Ndo ujiulize sasa nimeacha 4k halafu nikaongeza laki mbili kuchukua FullHD sio kwamba sina akili au sizijui screen resolutions.
Nilichoangalia DStv wanarusha matangazo yao 1080p resolution hii ni fullHD tu, Azam wao bado wako zama za mawe na HD, hakuna king'amuzi duniani kinachorusha matangazo 4k, yaani ni kwamba 4k ni sawa na kununia simu ya 5G halafu laini zote ni 3G unakuta mtu ana decoder ya azam halafu ananunua tv 4k basi anakuwa anatumia tv 4k kuangalia picha matangazo HD huu ni ujinga.
Sababu ilionifanya ninunue Samsung FHD halafu nikaacha Hisense 4k nilizijaribisha tv hizo mbili nikaweka chanel moja kingamuzi Cha DStv hapo matangazo yalikuwa yanarushwa kwenye 1080p resolution, maanayake SAMSUNG FHD ilicheza picha FullHD na Hisense 4k ilicheza picha FullHD, matokeo Hisense 4k ilifunikwa na SAMSUNG FHD ndo maana sikuona tabu kuongeza laki mbili kuchukua SAMSUNG FHD nikaacha Hisense 4k,
Tv ina miaka mitano haina shida wala sijutii, watu wakija home wanaishia tu kusema TV yako inaonyesha vizuri, cha kushangaza wanaoniambia hivyo tv zao ni 4k