Kati ya mahindi na alizeti kilimo kipi kinalipa?

Mkuu vipi mrejesho?
Mkuu mrejesho ni kama ifuatavyo;

Nauli 60,000
mifuko-100*700=70000
turubali=3*28000=84000
wavunaji =20000*10=200000
Kupiga piga nguvu kazi 70000
mashine ya kupukuchua 1500kwa gunia@80=120000
Usafirishaji mzigo baada ya kazi=1200*80=96000
Uhifadhi tsh 200000
MENGINEYO 150000
Jumla 1,050,000

Jumla ya garama zotekuanzia mwanzo mpaka mavuno ilikuwa 2,909,000/=

Mapato yalikuwa gunia 8 kwa ekari moja; kwa heka 10 ilikuwa gunia 80.
Nliuza kwa bei ya 70,000 mwishoni mwa june 70,000x80=5,600,000.

Faida halisi ilikuwa Tsh2,691.000.
 
Mkuu uliichoandika hapa hakina uhalisia mahindi ukitumia laki saba gharama AF uuze gunia bei hio hupati faida maisha alaf ekar moja huwezi pata gunia 25 kama ulivyo andika mm mwaka huu ndio navuna sasa hivi bei sio mbaya sana
 
hahah! Kwa msalaka ndugu mwaka huu ilinipa heshima nikarudi zangu na vibunda
 
Kila zao linalipa inategemea na soko pamoja na gharama za uzalishaji
 
Sasa kama mtaji ni mkubwa,faida inakuwaje kubwa tena?.
 
Duh!Ubarikiwe.
 
Kama hizi hesabu ziko sahihi kwanini watu wengi hukimbilia kulima mahindi na si alizeti? Mm Nina mashaka na hesabu zako!!! Mana tungekuwa hatuna changamoto ya mafuta nchini
Kaka!Wakulima wengi ni watu wasiyo na elimu sahihi ya kilimo cha hesabu.Mkulima yeye uangalia idadi ya magunia na siyo thamani ya zao husika.Hii ndiyo sababu ya mkulima kulima mahindi zaidi kwa sababu atavuna gunia nyingi ukilinganisha na gunia chache zipatikanazo katika alizeti.
 
Kilimo cha PDF hichi
 
NYIE!!!!kilimo kina faida sana ukiwa hauko field....ingia sasa ndo utajua songombingo zake!kilimo hakitak matarajio makubwa,utakufa mapema!
 
Tuko bize saivi tunapanda zetu pia Tunapalilia, wew tuachee kwanza tutaongea badae
 
Asante naomba kujuzwa alizeti inachukua mda Gani toka kupanda Hadi kuvuna??
 
Pole mkuu. Inategemea mbegu uliopanda msimu na uangalizi wa shamba lakini alizeti ina faida kubwa kuliko mahindi
 

Umechanganua vizuri lkn hapo kwenye kiasi cha mavuno cha alizeti hapajakaa sawa kwa uzoefu alizeti chotara waweza toa 7 mpaka 12 gunia za 60 to 70kg na kwa mbegy opv 4 to 7 za 65 to 70kg.
Lkn pia faida ya alizeti ni ukikamua mafuta na sio kuuza kama grain.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…