Kati ya Manyoni, Mpanda na Morogoro (Ifakara, Mvomero na Gairo) ipi sehemu ya kutoboa kimaisha?

Kati ya Manyoni, Mpanda na Morogoro (Ifakara, Mvomero na Gairo) ipi sehemu ya kutoboa kimaisha?

Kwa magonjwa ifakara na mvomero inaingoza hivyo kama target Yako ni kufanya biashara ya madawa panakufaa though wapo wafanya biashara wa bidhaa hiyo wengi.
Kuhusu majungu hata mvomero yapo sana tu make wenyeji ni wazigua.
Ifakara hakuna majungu na pia itategemea na sehemu utakayoishi make changamoto ni Barbara kipindi Cha masika ila ifakara, mlimba na (hasa)malinyi Pako poa sana!
 
Unasikia ila haujawahi fika mkuu ofcourse hata mimi nasikia pako vizuri mimi nipo pangani mkuu
Pangani na handeni zinaharibu sifa ya mkoa umwinyi mwingi,tafuta muda uende Kushoto kama kutalii huenda pakawa poa,na huenda uhamisho wake ukawarahisi
 
Pangani na handeni zinaharibu sifa ya mkoa umwinyi mwingi,tafuta muda uende Kushoto kama kutalii huenda pakawa poa,na huenda uhamisho wake ukawarahisi
Kabisa bora handeni kupo safi ila hiyo pangani kama wewe ni hustle utatamani kuondoka tu
 
Wakuu mimi ni mtumishi aisee huku niliko Tanga mambo magumu nahisi kutoboa itachukua muda sana wakuu sasa nataka nichague sehemu kama tatu hivi kati ya mkoa wa morogoro (Gairo, Mvomero au Ifakara), Mpanda na Manyoni ipi ni sehemu mzuri kutoboa? Wakuu hasa hasa kwenye kilimo na kuuza maduka ya madawa.

Mimi ni mtumishi wa Afya wizara ya tam
Nenda Ifakara
 
Kabisa bora handeni kupo safi ila hiyo pangani kama wewe ni hustle utatamani kuondoka tu
Pangani, Mwera, Kipumbwi na Sakura sio sehemu za kufanyia biashara watu wanafanya biashara kwa kuangaliana huyu mtu wa wapi .
 
Wale ni manamba kule hasa msimu huu wa kilimo wanaenda huko kwa makundi, japo ardhi bado ni kubwa
Wasukuma ndio wanaoibeba mikoa ya Rukwa na Katavi ndio wenye nguvu za kiuchumi kuanzia Majimoto,Kakese, Kiiando,Kalema hadi Mpunze ziwani. ukienda maeneo ya Kakese kukodi heka 1 ya kulima Mpunga ni kadri ya lak 2 hadi lak 3 wakati maeneo ya Kilosa na Mvomero unaweza kupata kwa 70 hadi laki 1
 
Unataka kuacha kazi au?
Kwamba ukihamia maeneo hayo kama mtumishi ndio unategemea utoke Kwa kufanya biashara ulizotaja?
Na kama utakuwa mtumishi utawezaje kusimamia hizo biashara vizuri na kikamulifu huku ukiwa mtumishi?
Embu fafanua usaidiwe.
Ila ningekushahuri ujaribu cope na mazingira unapoishi.
Kituo cha kazi ulipo sasa una mda gani?
 
Ndugu,kwa kilimo tazama wepesi wa usafirishaji kwenda sokoni mfano Gairo pamekaa vizuri sana.Baadhi ya maeneo ni mazito kwa sababu ya umbali kutoka saiti hadi sokoni.
Hii point ya muhimu sana
 
Wakuu mimi ni mtumishi aisee huku niliko Tanga mambo magumu nahisi kutoboa itachukua muda sana wakuu sasa nataka nichague sehemu kama tatu hivi kati ya mkoa wa morogoro (Gairo, Mvomero au Ifakara), Mpanda na Manyoni ipi ni sehemu mzuri kutoboa? Wakuu hasa hasa kwenye kilimo na kuuza maduka ya madawa.

Mimi ni mtumishi wa Afya wizara ya tam
Waarab wanaishi jangwani na wametoboa maisha, inategemea unataka kufanya nini
 
Back
Top Bottom