Kati ya matofali ya kuchoma na ya saruji unachagua yapi?

Mwishowe nimejikuta natoa hizo kauli, ukweli unaujua ila unataka kuleta pigo za wanasheria utafute ka angle kamoja kabadilishe context nzima, wewe ulipaswa kusomea sheria tu.

Sikuwa na lengo la kuku-blackmaili, kuwa na amani mimi nipo hapa kujadili hoja.
 
Mkuu narudia kusema hizi procedures ni kwenye commerical buildings na wale wa sky scrappers
Ghorofa nyingi za kuishi unazoona watu wamejenga kuholela bila hizo procedures. Of ourse procedures zinapaswa kufatwa lakini pamoja hazifuatwi bado wameweza kusimamisha hizo ghorofa na ndio hapo tulikua tumeanzia.
 
Thanks nami nimeelewa vyema tu nilikua naweka sawa hiyo paragraph yako ya kwanza😂😂
 
Ooooh hapo sasa nimekuelewa, kama ni hizo za kuishi na zile zinazojengwa kiholela pengine watu wanajenga tu bila kuzingatia hizo procedures, NI KWELI wanajenga hata mimi najua.

Ila mimi sikutaka kujadili ujenzi wa Ghorofa katika context ya kulijenga kiholela, mimi nilikuwa najadili as how inatakiwa kuwa kitaalamu, ndomaana hatukuelewana.

UWE NA USIKU MWEMA MKUU.
 
But sababu ya kufika huku ilikua ni je ghorofa litasimama, hapo ndio tulianzia bila hizo procedures za mwanzo ulizosema
 
Ukijenga kwa satandard zote ni imara ila zikitengenezwa kwa kubumba lazima zitakuwa za hovyo! sasa mtu tofali za saruji unatoa tofali 45 hadi 50 unategemea kweli zitakuwa nzuri? Jaribu kutoa 30 au 25 uone zitakavyotoka kama chuma
Sisi hapa Nyumba ya urithi mzee alijenga kwa saruji, tofali alinunua wapi sijui miaka ya 80 huko......
Kuta zipo ngangari kinoma msumari haupenyi Hadi concrete nail ndio zinapita kwa shida sana.
 
Za kuchoma ni imara zaidi.
 
Kule Kijijini kwetu tofali zinazotumika zaidi ni za kuchoma. Nami nyumba yangu nimejengea tofali za kuchoma ila nilipiga plaster, yaani nyumba iko poa sana. Halafu nikajenga nyumba ya Wazazi wangu kwa tofali za kuchoma, sikupiga plaster, nilifanya pointing. Nyumba inapendeza ni balaa.
 
hyo ratio bado ni famba, ratio sahihi ni 25:1, kuna mzungu ar alikuwa anafyatua kwa 20:1, tofauli linakaushiwa ndani kwenye unyevunyevu, ukienda kununua anakupa usafiri, ukifika site hakuna mambo ya kupakua moja moja, kitu inapigwa tip, likimeguka hata moja anakurudishia hela anarudi na tofali lake
 
Mkuu you have nailed. Mimi nimesoma Ifunda, yale Mabweni yetu yalijengewa tofali zilizoandaliwa kwa kuchomwa hapo Ihemi miaka hiyo ya 1920 lakini hadi leo ni kama jengo la jana tu. Kuna kipindi alikuja Wazir Mkuu Mstaafu Marehemu Mzee Kawawa hapo Ihemi akawahamasisha matajiri wajenge Kiwanda cha Vigae maana udongo uliopo hapo ni mzuri kwa matofali ya kuchomwa pamoja na vigae. Kwa kipindi hicho matajiri walikuwa hawapendi sana ishu za uwekezaji sababu ya masuala ya ujamaa hivyo kiwanda kikaishia katika maono tu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…