Ninadhani unasababisha ubishani usio na sababu. Mtoa post aliuliza kiujumla. Na baadhi ya wachangiaji tumemjibu kuwa kama mambo yatafanyika kikanuni, kwa tofali zote, kuchoma ni namba moja. Wewe post hii ndo umeonesha kuwa kumbe unakiri la kuchoma ni kiboko mradi tu viwango viwepo. Ile hoja yako ya mwanzo hadi nikakujibu vile ni kwa vile uliongea kiujumla tu. Yani kama unafundisha basi mwanafunzi anaelewa la kuchoma halifai, na sababu ni vile huoni watu wakijengea. Hii ni dhambi aisee!
Halafu bado hoja zako si madhubuti sana. Eti za kuchoma hutumiwa na masikini. Umeipata wapi hii? wabongo baadhi kwa kutojua ama sababu za kimazingira ndo huchagua saruji. Na wanatumia matofali ya kiwango cha chini mno. tofali unakuta 1:40. ndo majengo yaliyojaa miji yetu hasa Dar na maeneo jirani. Sababu kubwa kwa hapa kwetu watu kutumia ya kuchomwa ama saruji ni mazingira. Mpaka mkazi wa Dar pale magomeni apate tofali la kuchomwa litamfikia kwa kiasi gani? Hali hii ni tofauti ukiwa Iringa. Yale majumba ya wazee vibopa wa Kikinga kule Kihesa na Gangilonga yote ni tofali za kuchomwa. Kuna nyumba zimejengwa Dar mwaka jana, lakini haziingii kwa nyumba zile aisee zenye miongo kadhaa. Kakague chuo kama Mkwawa, sekondari kama Ifunda n.k. kisha njoo utuambie ule ni umasikini ama la.
Cha ajabu, ukizungumza kuhusu saruji, unataja standard hiyo ya 1:25, na hzi za kuchomwa pia zina viwango vyake, vikifikiwa ni bora zaid ya saruji. Na wangapi bongo wanajengea tofali za 1:25? Tumuogope Mungu aisee!