Chikuvi2021
JF-Expert Member
- Aug 3, 2021
- 491
- 551
-Waziri wa Tamisemi naye,asimamie vizuri zoezi la anuani za makazi hususani mijini.Tangu iingie awamu ya Tano Mtendaji wa serikali ni mmoja tuu.
Hao wengine ni watu waliobahatika kupata fursa za kula Bata Kwa Kodi ya Watanzania.
Mtendaji ni Rais TU labda kidogo na Waziri Mkuu.
Mawaziri walikua ni Wanne TU mpaka Sasa :-
Lowasa (Maji ) aliibuliwa na Mkapa.
Lukuvi ( Ardhi) aliibuliwa na Kikwete
Magufuli (Ujenzi ) aliibuliwa na Mkapa.
Mrema (Mambo ya ndani) aliibuliwa na Mwanyi.
Magufuli hakuibua Wazirj na Mtendaji mwenye uwezo mpaka anaondoka Duniani!
Mama Samia mpaka Sasa Hana Waziri zaidi ya yeye Mwenyewe kuupiga mwingi lakini Hana wafungaji, ni sawa na Kocha asiye na wachezaji wa uhakika anayeamua kuwa Mchezaji kumsaidia kipa , beki na mshambuliaji; wakati huo huo akiwa kocha. Kuna Mchezaji wa Simba zamani alikua anaitwa Hassan Hafifu alikua anacheza na kumiliki uwanja mzima. Alikua ni kocha Mchezaji.
Angalau kidogo Waziri ambaye akijipanga vizuri anaweza akaimudu kazi yake ni Nape mpaka Sasa angalau anaonyesha kuwa anaweza japo siasa za uchama zimemzidi.Na pia Bado anakashfa ya kushiriki katika kujenga mifumo ya dhulma za kisiasa na kufanya viongozi wasiofaa kupata fursa za kutangazwa washindi Kwa nguvu wakati wa uchaguzi. Hii laana aitubie ili apate Kibali.
Nape akiweka pembeni uchama na kuweka mbele maslahi ya Nchi atakua Waziri Bora sana. Hana Kashifa Wala tamaa za kujimilikisha Mali za dhulma dhulma.
Makonda akirudia shule na kusoma Kwa cheti chake Cha Jina lake halisi la Albert na kuondoa ubini wa Bashite mana Bashite limekua kama msamiati mpya wa mtu mwenye vyeti feki ,atakua ni Kiongozi mzuri aondokana na chuki za kivyama na ajifunze Nini maana ya Demokrasia na uhuru na haki za binadamu kuishi.
Mtu pekee anayeweza kuwa Waziri akàcha Alama ndani ya CCM Kwa Sasa ni Antoni Mtaka RC Dodoma.Napendekeza Anton Mtaka ateuliwe kuwa Mbunge na Kisha apewe Naibu Waziri Wizara ya ujenzi amsaidie Mbarawa kusimamia Hawa TARURA na Tanroad Wajenge Miundo Mbinu za vijijini Kwa Kasi na Kwa viwango .
Gwajima na Mwenzake
Ndalichako
Wanapaswa kuwekwe kwenye kamati ya Elimu na Afya bungeni lakini sio kuwa Mawiri.
Ningekua Rais ningeweka nafasi za uwaziri wazi watu waombe na kila mmoja aseme anaweza kuongoza wizara Gani na ataje changamoto zake na namna atakavyoshughulika nazo. Pawe na kiapo na ajiwekee mwenyewe muda wa kuyatekeleza hayo na asipoyatekeleza achukuliwe hatua Kali ikiwa ni pamoja na kuchunguzwa na akibainika alizembea Kwa sababu ya kushirikiana na mafisadi basi afilisiwe kabisa. Anayefanya vizuri apewe bonasi ya mil. 500 kila Baada ya miaka mitano na wananchi ndio watatoa tathmini ya Waziri Bora. Waziri atalazimika kuwa mbunifu na kuongeza uzalishaji na kubana mianya ya matumizi mabaya ya wizara.
Leo hii ukipita Huko Halmashauri ni vikao TU wiki nzima sijui pesa wanapata wapi za vyakula ,maji na soda halafu Waziri yupo, viongozi wa Chama kwenye Wilaya wapo wanaangalia TU pesa za wananchi zinaliwa Kwa Tenda za kuuza chakula na vinywaji Kwa Mwezi vikao ni zaidi ya siku kumi. Matumizi mabaya ya serikali. Waziri Muhusika apumzike mana hii nchi sio ya ukoo wake Wala ya Babu yake kwamba uwaziri ni urithi wake. Yes. Mawaziri wasiofaa wapumzishwe.
-wenyeviti wa Serikali za mitaa mijini wanatengeneza mitaa ndani ya mtaa Jambo linaloleta confusion,
-kwa mujibu wa Sheria za Tamisemi,kwa mijini Kuna mitaa,kata,tarafa na wilaya.
juzi nilimtembelea rafiki yangu wilaya ya Temeke-mtaa wa vituka kata ya yombo vituka,eneo ambalo halijapimwa.
-Mtaa wa vituka umegawanywa mitaa zaidi ya 50 na imewekwa majina ya wajumbe wa mashina au watu.
-Swali la kujiuliza,ni kwamba,je Mtaa wa vituka umekufa na kuzalishwa mitaa mingine midogo midogo?
-Mitaa midogo midogo inakuwa na nyumba chache Sana,Kwani Serikali haikuweka vigezo/miongozo ya idadi ya nyumba zinazotakiwa kuwepo ili kufanya mtaa.
-Kuna nyumba moja ambayo ipo kwenye Kona inawekwa kwenye mitaa miwili na namba mbili tofauti.
- viongozi wa Serikali za mitaa wengi wao hawakuwashirikisha wananchi, zoezi la anuani za makazi kutoa maoni na mapendekezo ya majina ya mitaa .
-Serikali au Waziri wa Tamisemi achukue hatua ya kutoa miongozo ya jinsi ya kutekeleza zoezi la anuani ya makazi, vinginevyo watendaji wa Serikali za mitaa watakuangushia jumba bovu mambo yakiharibika.
Ushauri
1).Kwa kuwa mijini
zoezi la anuani za makazi,tuwe tunaita barabara/njia badala ya kuita mitaa kwa maeneo ambayo hayajapimwa au -Tuite Location, na Sub-location-(Kwa maneno ya kiswahili)
2)Kwa mfano Mtaa wa vituka barabara ya kwanza,au barabara ya 15 nk.
3). Wenyeviti wa Serikali za mitaa wawashirikishe wananchi wote kutoa maoni au kutoa elimu kwa wananchi badala ya kufanya maamuzi bila ushirikishaji
4). Waziri atoe mwongozo kuhusu nyumba ngapi zinafanya mtaa na kama ametoa basi wasaidizi wake wafuatilie.
- kuna makosa mengi yameanza kujitokeza katika utekelezaji wa anuani za makazi huku mitaani.
5). Kwenye zoezi la sensa,makarani wa sensa waende kwenye nyumba kuhesabu,watu badala ya wananchi kwenda kwenye Serikali mitaa kujiandikisha