Kati ya Mawaziri hawa; Nani unadhani atafuata kurejesha nyumba ya Serikali hivi karibuni?

-Waziri wa Tamisemi naye,asimamie vizuri zoezi la anuani za makazi hususani mijini.
-wenyeviti wa Serikali za mitaa mijini wanatengeneza mitaa ndani ya mtaa Jambo linaloleta confusion,
-kwa mujibu wa Sheria za Tamisemi,kwa mijini Kuna mitaa,kata,tarafa na wilaya.
juzi nilimtembelea rafiki yangu wilaya ya Temeke-mtaa wa vituka kata ya yombo vituka,eneo ambalo halijapimwa.
-Mtaa wa vituka umegawanywa mitaa zaidi ya 50 na imewekwa majina ya wajumbe wa mashina au watu.
-Swali la kujiuliza,ni kwamba,je Mtaa wa vituka umekufa na kuzalishwa mitaa mingine midogo midogo?
-Mitaa midogo midogo inakuwa na nyumba chache Sana,Kwani Serikali haikuweka vigezo/miongozo ya idadi ya nyumba zinazotakiwa kuwepo ili kufanya mtaa.
-Kuna nyumba moja ambayo ipo kwenye Kona inawekwa kwenye mitaa miwili na namba mbili tofauti.
- viongozi wa Serikali za mitaa wengi wao hawakuwashirikisha wananchi, zoezi la anuani za makazi kutoa maoni na mapendekezo ya majina ya mitaa .
-Serikali au Waziri wa Tamisemi achukue hatua ya kutoa miongozo ya jinsi ya kutekeleza zoezi la anuani ya makazi, vinginevyo watendaji wa Serikali za mitaa watakuangushia jumba bovu mambo yakiharibika.

Ushauri
1).Kwa kuwa mijini
zoezi la anuani za makazi,tuwe tunaita barabara/njia badala ya kuita mitaa kwa maeneo ambayo hayajapimwa au -Tuite Location, na Sub-location-(Kwa maneno ya kiswahili)
2)Kwa mfano Mtaa wa vituka barabara ya kwanza,au barabara ya 15 nk.
3). Wenyeviti wa Serikali za mitaa wawashirikishe wananchi wote kutoa maoni au kutoa elimu kwa wananchi badala ya kufanya maamuzi bila ushirikishaji
4). Waziri atoe mwongozo kuhusu nyumba ngapi zinafanya mtaa na kama ametoa basi wasaidizi wake wafuatilie.
- kuna makosa mengi yameanza kujitokeza katika utekelezaji wa anuani za makazi huku mitaani.
5). Kwenye zoezi la sensa,makarani wa sensa waende kwenye nyumba kuhesabu,watu badala ya wananchi kwenda kwenye Serikali mitaa kujiandikisha
 
Hapo Kwa Anthony Mtaka umeupiga mwingi, naomba Sana mama ikimpendeza atuletee huyu mzalendo.
 
Ningekua Rais ningeweka nafasi za uwaziri wazi watu waombe na kila mmoja aseme anaweza kuongoza wizara Gani na ataje changamoto zake na namna atakavyoshughulika nazo. Pawe na kiapo na ajiwekee mwenyewe muda wa kuyatekeleza hayo na asipoyatekeleza achukuliwe hatua Kali ikiwa ni pamoja na kuchunguzwa na akibainika alizembea Kwa sababu ya kushirikiana na mafisadi basi afilisiwe kabisa. Anayefanya vizuri apewe bonasi ya mil. 500 kila Baada ya miaka mitano na wananchi ndio watatoa tathmini ya Waziri Bora. Waziri atalazimika kuwa mbunifu na kuongeza uzalishaji na kubana mianya ya matumizi mabaya ya wizara.


KATIBA YA WARIOBA ILIONA MBALI SANA UMEPIGA MULE MULE. Hii ni comment bora kabisa Jumapili ya Leo.
 
(1)JK. Nyerere.
(2)Edward Moringe Sokoine
(3)Augustine Mrema.
(4)Edward Ngoyayi Lowasaa.
(5)John Pombe Magufuli.
4 NO

Wapo wenye data zake wakiziweka hapa utaacha kumtaja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…